Pages

Pages

Thursday, February 9, 2012

JACKLINE WOLPER ATAFUNA FEDHA ZA KIGOGO WA BENKI

 SIRI iliyokuwa inatafutwa kwa muda mrefu juu ya maisha ya staa wa filamu za kibongo, Jackline Wolper, sasa imevuja ambapo inadaiwa kuwa anatembea na kigogo wa Bank kubwa Tanzania, ambaye familia yake inaishi nchini Marekani.

Awali kabla ya uchunguzi kufanyika juu ya fedha anazozipata msanii huyo kupitia filamu, ili kujua kama zinaweza kumruhusu kufanya matanuzi makubwa ambayo amekuwa akiyafanya.


Msanii huyo anasifika kwa matumizi makubwa ya fedha lakini kiwango chake cha fedha anacholipwa katika filamu anazocheza si kikubwa cha kumfanya kuishi kama wasanii nyota wa
Marekani.

Uchunguzi huo ulibaini kuwa msanii huyo amekuwa akipewa shilingi milioni 3, kwa siku kwa ajili ya matumizi na kigogo huyo wa bank yenye zamani kubwa Tanzania.


M wandishi
hakusita kuzungumza na Wolper, ili kupata maneno yake, ambapo alisema kuwa hakuna mtu anayehusika juu ya mapenzi yake na kigogo huyo.

Alisema kuwa hata hivyo siri hiyo imevuja lakini bado ataendelea kuwa na siri nzito juu ya maisha yake kwani hakuna mtu ambaye anaweza kujua nini anachokifanya katika maisha ya kila siku.


“Mimi najua kuna watu wanapenda kutoa habari za uongo lakini naweza kusema kwamba hakuna anayeweza kuwa na siri ya maisha yangu nina siri nzito kuliko mtu yeyote,”
alisema.

Msanii huyo alisema fedha zake anazolipwa katika kila filamu anayocheza inamsaidia katika maisha yake kawaida na kutembea na kigogo huyo haimanishi ndiye anayemuweka mjini.

No comments:

Post a Comment