Pages

Pages

Tuesday, February 7, 2012

MAUAJI YA RAIA YAENDELEA NCHINI SYRIA

Mji wa Homs nchini Syria imekuwa ukitikiswa na mashambulio mazito ya silaha, wakati majeshi ya Syria yakiongeza nguvu za kushambulia mji huo. Wanahabari waliyeko huko wanasema kuna milio inayofuatana, katika shambulio kali zaidi katika kipindi cha miezi 11 ya maandamano. Rais wa Marekani Barack Obama amesema ni muhimu kumaliza mzozo huo bila kuingilia kijeshi. Wakati huohuo, Urusi na Uchina zimetetea kura yao ya veto katika muswada wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, hatua ambayo imewakasirisha mahasimu wa Rais Bashar al-Assad. Mji wa Homs, moja ya ngome kubwa zinazopinga utawala wa Bw Assad, umekuwa ukishambuliwa na majeshi ya serikali kwa siku kadhaa.   Waasi wanadai kuwa mashambulizi ya majeshi ya serikali yameteketeza hospitali katika wilaya ya Baba Amr na kusababisha vifo.

No comments:

Post a Comment