Pages

Pages

Wednesday, February 15, 2012

TWANGA PEPETA BADO WAMO, WASUGUA VISIGINO MWANZO MWISHO USIKU WA WAPENDANAO (VALENTINE DAY) EQUATOR GRILL

Mwimbaji wa bendi ya African Stars Janet Isinika kushoto akicheza pamoja na wanenguaji wa bendi hiyo katika onyesho la usiku wa wapendanao Valentine Day lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ali jijini Dar es salaam, Wapendanao walijumuika na wapenzi wao kusherehekea siku hiyo ambayo imekuwa ikijichukulia umaarufu siku hadi siku hapa nchini Tanzania.
Asha Baraka Mkurugenzi wa African Stars akiongea na wadau wa bendi hiyo wakati wa onyesho la bendi yake usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi.
Hii ni staili ya kulia na kubembelezwa kutoka kwa wana wa Kutwanga na Kupepeta African Stars.
Janet Isinika akicheza na mmoja wa wa wanenguaji wa kiume wa bendi ya African Stars.
Mdau Mohamed Jumakushoto akiwa na rafiki yake Muhsin nao walikuwepo kuwashuhudia wana wa Kutwanga na Kupepeta katika usiku wa wapendanao usiku wa kuamkia leo.
Wapenzi wa bendi ya African Stars wakijimwaga kusakata rhumba ukumbini wakati bendi hiyo ilipokuwa ikifanya vitu vyake usiku wa kuamkia leo.
Vimwana wa bendi ya Africana Stars wakionyesha ujuzi wao jukwaani wakati bendi yao ilipokuwa ikifanya vitu vyake kwenye ukumbi wa Equator Grill usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment