Pages

Pages

Thursday, February 16, 2012

WAFUNGWA 300 WATEKETEA KWA MOTO HONDURAS

Wanajeshi, polisi na waandishi wa habari wakijihami na machafuko yaliyotokea mara baada ya wananchi kuvamia gereza.
Takriban wafungwa 300 wameuwawa katika moto ulioteketeza jela moja nchini Honduras kwa mujibu wa maafisa wa serikali.
Wananchi waliochachamaa walivunja geti la lango kuu la gereza na kuingia ndani.
Wengi wao waliteketea au kukosa hewa katika seli zao za jela ya Comayagua, kaskazini mwa mji mkuu Tegucigalpa.

Maafisa wa serikali wanasema imethibitishwa takriban 300 wamekufa lakini wengine 56 kati ya wafungwa 853 katika gereza hilo hawajapatikana na inadhaniwa wameteketezwa.

Jamaa wa wafungwa hao walipambana na polisi pale walipojaribu kuvamia jela hiyo wakitafuta maelezo zaidi ya majaaliwa ya watu wao.
Polisi walipaswa kufyatua risasi hewani na kutumia gesi ya kutoa machozi. Uchunguzi unaendelea kuhusu chanzo cha moto huo kama ulisababishwa na hilitalfu katika nyaya za umeme ama zilichochewa na ghasia za wafungwa.

Rais Lobo wa Honduras ameahidi uchunguzi kamili ulio wazi na kusema hillo ni janga lisilokubalika.

Alisema wakuu wa magereza wa kitaifa na wa eneo la moto huo watasimamishwa kazi wakati uchunguzi ukiendelea.

No comments:

Post a Comment