Pages

Pages

Friday, February 17, 2012

WIMBI LA AJALI UPYA MKOANI MBEYA, ABIRIA 50 WANUSURIKA KIFO.

 Askari wa Jeshi la Polisi usalama wa barabara wakitazama basi aina ya Scania lenye nambari za usajili T 281 AAR mali ya kampuni ya Happy Nation lilokuwa likitokea Mkoani Mbeya kwenda jiji la Dar es salaam kuacha njia na kupinduka katika eneo la Inyala mkoani hapa ambapo abiria 50 wamenusurika kifo.
 Pichani ni baadhi ya abiria wakitizama basi hilo baada ya kupinduka katika eneo la Inyala na abiria 50 kunusurika kifo.
 Baadhi ya abiria wakiitafakari ajali hiyo, baada ya kutoka salama salimini, licha ya mmoja wao kujali zaidi mizigo kwa kuitoa ndani ya basi aina ya Scania lenye nambari za usajili T 281 AAR mali ya kampuni ya Happy Nation lilokuwa likitokea Mkoani Mbeya kwenda jiji la Dar es salaam kuacha njia na kupinduka katika eneo la Inyala mkoani hapa ambapo abiria 50 wamenusurika kifo.
Baadhi ya abiria wakiitoa mizigo ya baada ya basi aina ya Scania lenye nambari za usajili T 281 AAR mali ya kampuni ya Happy Nation lilokuwa likitokea Mkoani Mbeya kwenda jiji la Dar es salaam kuacha njia na kupinduka katika eneo la Inyala mkoani hapa ambapo abiria 50 wamenusurika kifo.
 Baadhi ya mizigo iliyotolewa na kuwekwa chini baada ya basi aina ya Scania lenye nambari za usajili T 281 AAR mali ya kampuni ya Happy Nation lilokuwa likitokea Mkoani Mbeya kwenda jiji la Dar es salaam kuacha njia na kupinduka katika eneo la Inyala mkoani hapa ambapo abiria 50 wamenusurika kifo.
Askari wa Jeshi la Polisi usalama wa barabara akitazama basi aina ya Scania lenye nambari za usajili T 281 AAR mali ya kampuni ya Happy Nation lilokuwa likitokea Mkoani Mbeya kwenda jiji la Dar es salaam kuacha njia na kupinduka katika eneo la Inyala mkoani hapa ambapo abiria 50 wamenusurika kifo.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya.)
******
 Habari na Mwandishi wetu.
Zaidi ya abiria 50 wa basi la kampuni ya Happy Nation lilokuwa likitokea Mkoani Mbeya kwenda jiji la Dar es salaam wamenusurika kifo baada ya basi aina ya Scania lenye nambari za usajili T 281 AAR kuacha njia na kisha kupinduka katika eneo la Inyala mkoani hapa.

Tukio hilo lilitokea jana majira saa moja asubuhi jana,basi lilo kuacha njia na kupinduka baada ya kujaribu kulipisha basi la kampuni ya Nganga lililokuwa mbele yake katika mtelemko wa Inyala karibu na kituo cha mafuta cha Tazama  Pipeline kilichopo Shamwengo  Mbeya Vijijini 

Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa basi hilo na hivyo dereva wa basi hilo na kushindwa kulimudu na hivyo kupinduka na kusababisha majeruhi,  ambapo watu 10 wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya wakipatiwa matibabu.

Dereva wa basi  hilo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

No comments:

Post a Comment