Pages

Pages

Monday, March 12, 2012

IZZLE BUSINESS ANUFAIKA NA MAUZO YA T-SHIRT APATA 20 ML

MSANII wa muziki wa kizazi bongo, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Business’, amesema kuwa mtaji alioanza nao katika kufungua duka lake la nguo lilipo mkoani Mbeya ni Sh mil 5, ambapo hadi sasa limeweza kumwingizia kiasi cha sh mil 20.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, msanii huyo alisema kuwa anamshukuru mungu kwani wateja wake wameweza kulipokea kwa roho moja na kumpa sapoti kubwa.

Alisema kwua sambamba na watu kulipokea kwa roho moja bado anajitahiji kununua nguo zinazoenda na wakati ili mashabiki pamoja wateja wake waweze kuvaa nguo halizi zilipokwenye soko kwa sasa.

“Wateja wangu huwa nawaambia kwamba ni lazima nguo ambazo tunavaa ziwe zile amabzo zipo kwenye soko kwa sasa na hilo ndilo linalonipa wateja wengi ambao hata hivyo wanakubali nguo zinazopatikana,” alisema.

No comments:

Post a Comment