Pages

Pages

Saturday, March 17, 2012

KAJALA KIZIMBANI TENA..!!

MSANII wa filamu nchini Kajala Masanja na mumewe Faraja Chambo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kula njama, kuhamisha umiliki wa nyumba na kutakatisha fedha haramu. Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai kuwa mwaka 2010 , Kajala na Chambo walikula njama ya kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala wilaya ya Kinondoni kinyume na kifungu cha 34 cha sheria ya rushwa ya mwaka 2007 sura ya 11. Swai alidai kuwa Aprili 14, 2010 jijini Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja kinyume na kifungu cha 34 (2)a(3) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa walihamisha umiliki wa nyumba hiyo iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam. Alidai kuwa siku hiyo ya Aprili 14,2010 washtakiwa hao ambao ni mtu na mkewe walifanya uhamisho wa umiliki wa nyumba hiyo iliyopo Kunduchi Salasala ambayo ilipatikana kutokana na fedha haramu. Wakati kesi hiyo ikiendelea Kajala pekee ndiyo aliyokuwepo mahakamani hapo na mumewe Chambo ambaye anakabiliwa na kesi nyingine za kutakatisha fedha haramu mahakamani hapo hakuwepo. Katika kesi hiyo, Kajala anatetewa na Wakili Alex Mgongolwa ambaye alidai mahakamani hapo kuwa Wakili huyo wa Takukuru , Swai hana mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba hati ya mashtaka inamapungufu. Akijibu hoja: Wakili Swai alidai kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliteua mawakili wa Takukuru chini ya Government Notice (GN) 168 ya mwaka 2010 na kuwaruhusu kuendesha kesi zisizokuwa za rushwa na kwamba katika uteuzi huo yeye alikuwa ni mmojawapo. Hivyo anauhalali wa kuendelea kuendesha kesi hiyo. Hakimu Fimbo ameiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20, mwaka huu atakapotoa uamuzi juu ya hoja hizo.

No comments:

Post a Comment