Pages

Pages

Tuesday, March 6, 2012

LULU KUMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE KWA WAZAZI

  Mwana bongo movie mwenye vituko vya kila namna ndani ya kiwanda cha filamu Tanzania,Elisabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’, baada ya kimya ameibuka na kudai kuwa anatarajia kumtambulisha mpenzi wake kwa wazazi wake ili aweze kuishi naye kama mume.

Chanzo cha habari
kilipata habari hizo kutoka kwa mmoja wa marafiki wa msanii huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe, alidai kuwa kuna mwanaume ambaye anauwezo kifedha ndiye alimpagawisha hadi kutaka kumtambulisha kwa wazazi wake.

  Rafiki huyo alisema kuwa mwanaume huyo siyo mkubwa kiumbo hata kiumri, ingawa hapatikani nchini mara kwa mara kutokana na biashara zake za nje ya nchi.


  “Wiki iliyopita tulikuwa naye sehemu moja na akatumbulisha na kwa wanavyoonekana wanapendana ingawa siwezi kumsemea mtu,”
alisema mdada huyo.

 Hata hivyo mwandishi wa habari hizi, hakuona kitu cha busara kama asipopata kauli kutoka kwa
Lulu, ambapo naye alipopatikana alisema kuwa anafikiria kuimtambulisha mwanaume huyo ili aweze kuishi naye kama mume.

  Alidai kuwa baada ya harakati kibao za mapenzi ambazo kipindi cha nyuma sasa amefungua kurasa mpya katika suala zima la mahusiano.

No comments:

Post a Comment