Pages

Pages

Thursday, March 8, 2012

WAZIRI WA AFYA KUJIUZURU ILA SI KWA SHINIKIZO LA MADAKTARI

Waziri wa Afya Dr Haji Mponda amesema yeye atajiuzulu ili kuokoa roho za watanzania ambao wataathirika na mgomo mpya wa madaktari na si kwa shinikizo la madaktari hao! Hayo aliyasema jana usiku kwenye kikao cha dharura cha baraza la Mawaziri cha kujadili mgomo mpya wa Madaktari na Manesi! Hata hivyo Mponda ametoa rai kwamba watanzania wawe makini sana na jinsi watu wanavyotumia migogoro kwa maslahi yao binafsi huku wakisababisha maafa makubwa kwa raia wasio na hatia, pia aliongeza kwa kusema kuwa kama wanataaluma wataingia kwenye ushabiki wa siasa nchi itaingia kwenye mgogoro mkubwa na kudhoofisha ustawi wa taifa letu!

No comments:

Post a Comment