Pages

Pages

Thursday, March 8, 2012

WEMA SEPETU NA SKENDO YA KUIBA MUME WA MTU

      Wema Sepetu.
  Gari inayomilikiwa na Wema Sepetu kwa madai ya habari za udaku kununuliwa na kibopa huyo.
Baada ya kuletewa fujo weekend iliyopita na mwanamke anaedai muigizaji Wema Sepetu amemuibia mume, leo mrembo huyo (Wema) ameamua kuzungumzia upande wake ambapo kama haukuingia. juzi march 5 kulikua na stori ya huyo mwanamke kumfanyia fujo Wema baada ya kumkuta yeye na wasanii wenzake ndani ya Pub ambayo inamilikiwa na mwanamke huyo.

Wema amesema “kwanza mimi mwenyewe nilishtuka sana, nilikua natafuta location ya kucheza movie yangu kwenye mgahawa, nikawa nimepaki nje kutoka na kurudi nikamkuta mwanamke ndani ya gari jeupe limepaki pembeni yangu siijui wala huyo mwanamke simjui nikamchukulia kama mmoja wa haters, akaanza kufanya fujo wakati mimi huwa siwezi fujo, nikajitahidi kutoka eneo la tukio na kupiga simu polisi na kuja kumchukua huyo mwanamke na kwenda polisi Osterbay”

“Kiukweli sitembei na mwanaume wake, sitembei na mume wa mtu……. alafu yule ni mwanamke mtu mzima sana hawezi kugombana na mimi, mi mtoto mdogo akitaka aje na uthibitisho, alafu anasema gari ninayotembela ni yake? gari ni yangu mpaka kazi ninazo mimi huo ni ujinga na ndio maana siwezi nikaachia hii kitu iende hivyo hivyo tu kama anavyotaka yeye” – Wema

“Kama kweli ningekua namchukulia mwanaume wake sidhani kama ningekua nimefikishana nae hapa tulipofika manake ningekua namuogopa, sasa simuogopi na afanye chochote anachotaka kufanya, waniache na maisha yangu nimekaa kimya mtoto wa watu wananifatafata, nikisema watasema nimesema, waniache basi mi mwenyewe nina maisha yangu ya kuishi” hayo ni maneno ya  Wema ambae pia amekataa na kuapa kwamba hajawahi kutumia bili za milioni 1.5 mpaka mbili kwenye baa ya huyo mwanamke, huku ikidaiwa kwamba bili hizo zimekua zikilipwa na huyo pedeshee ambae ni mume wa mwanamke mwenye pub.

Jana mmoja kati ya marafiki wa Wema akiwa ni mdogo wake na mke wa pedeshee huyo, alikiri kwamba urafiki wake na Wema umevunjika baada ya kugundua anatoka kimapenzi na mume wa dada yake (yani mume wa mwanamke aliemfanyia Wema fujo)

No comments:

Post a Comment