Pages

Pages

Sunday, April 15, 2012

MISS UTALII KINONDONI 2012 KUFANYIKA SUNCIRO

Shindano la kumpata Binti wa Utalii Kinondoni 2011/2012(Miss Utalii Kinondoni 2011/2012 ngazi ya wilaya limepangwa kufanyika katika ukumbi wa kisasa na Club ya kimataifa ya Sinsiro,iliyoko Shekilango Sinza.Shindano hilo limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 25 Mei 2012 na kushirikisha mabinti 25 kutoka katika majimbo yote ya wilaya ya Kinondoni.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa Miss Tourism Tanzania Organisation wilaya ya Kinondoni Pius Yalula,ambao ndio waratibu na waandaaji wa shindano hilo, washiriki wote wanatarajia kuanza kambi ya mazoezi katika ukumbi huo siku ya Jumatatu Mei 1,2012. Miss Utalii Kinondoni 2010/2011 Sophia Dioa ambaye pia ni Miss Utalii Dar es Salaam 2010/2011 na Miss Utalii Tanzania 2010/2011.

Piusi Yalula alibainisha kuwa ni mpango mkakati wa Miss Tourism Tanzania organisation mwaka huu, wa kuwafuata watanzania hususani vijana katika maeneo yao ya burudani,ili kuwahamasisha juu ya utalii wa ndani. 
Ndio maana fainali za mwaka za Miss Utalii Kinondoni ,tumeamua kuzifanyia katika Club ya Sunciro, ambako tunaamini kuwa vijana na watu wa rika mbalimbali wanapenda kwenda katika kumbi na club za aina hiyo kwa ajili ya burudani na mapumziko ya wikendi.

No comments:

Post a Comment