Pages

Pages

Monday, April 16, 2012

RAMBIRAMBI ZA MSIBA WA KANUMBA ZACHACHULIWA WENGI WANEEMEKA NA KIFO CHAKE

UONGOZI wa Bongo Movie uliohusika na uratibu wa shughuli za mazishi ikiwemo michango katika msiba wa msanii Steven Kanumba, umeingia kwenye kashfa nzito.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka ndani ya familia ya Kanumba, kamati hiyo imedaiwa kufanya uchakachuaji wa michango hiyo inayokadiriwa kuwa mamilioni ya fedha, achilia mbali
vitu kadhaa, yakiwemo magunia 32 ya mchele.
Chanzo hicho kimeidokeza blog hii kuwa, dalili za hali hiyo zilianza kujitokeza mapema kabisa pale mwanandugu mmoja alipoenguliwa kwenye kamati hiyo, kwa kile kinachoelezwa, kamati hiyo kufanya jukumu hilo kwa uhuru zaidi.
Dalili nyingine, ni kitendo cha wajumbe wa Kamati hiyo kutoweka baada ya mazishi hadi walipofika nyumbani kwa marehemu Alhamisi usiku.
Kwamba, pamoja na mambo mengine, kwenye kikao kilichofanyika siku hiyo kati
ya wanandugu na kamati hiyo, Mama Kanumba amezuia kuzungumzia suala la michango.
 “Mama Kanumba ametakiwa asiseme lolote kwa Waandishi wa Habari kuhusu michango… kaelezwa kama atafanya hivyo, huenda asipate kitu kabisa,” alisema ndugu huyo. 
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Kamati hiyo imetoa onyo hilo kwa vile tangu kwisha kwa maziko ya Kanumba, wamekuwa wakipata usumbufu wa simu watu kuulizia kilichokusanywa na kilichobaki.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, baada ya kamati hiyo kukutana na wanafamilia kwa mara ya kwanza baada ya ukimya mrefu, ilisema michango yote ni sh mil 51.
Kati ya fedha hizo, gharama za mazishi ni shilingi mil 48 huku kukiwa na deni la sh
mil 2 za ukarabati wa barabara Leaders kutokana na uharibifu uliofanywa na waombolezaji.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, walipohoji fedha zilizochangwa kupitia M-pesa kupitia namba ambayo ilitangazwa, walielezwa ilipatikana sh 20,000 tu.
Kilisema, kiasi hicho ni kiduchu mno kwa sababu mashabiki wa Kanumba wa Mwanza pekee, walichanga sh 300,000.
Kilidokeza kuwa, pia kulikuwa na gunia 32 za mchele zilitotolewa na msamaria, hazijulikani zilipokwenda.
“Licha ya kutolewa gunia 32 za mchele, hazijulikani zipo wapi…. fikiria hata mfiwa, anakosa hata gunia moja la kwenda kuanzia maisha mapya bila mwanaye,” kilidokeza chanzo hicho.  
Kilipoulizwa kwanini hawakuweka ndugu kwenye kamati hiyo tangu mapema, kilisema alikuwemo, lakini akaenguliwakwa kwa zengwe.
Uratibu wa msiba huo ulikuwa chini ya Kamati iliyokuwa chini ya Gabriel Mtitu na wajumbe kama Ray, Cloud, Steve Nyerere, Hapines Magese, Mtitu William, Jacob Steven na wengineo.
Sayari ilipomtafuta Mtitu kwa njia ya simu jana, alisema kutokana na usumbufu ambao wanaupata kwa wengi kutaka kujua juu ya michango hiyo ya msiba, Kamati yake imeamua kukutana na waandishi wa Habari kesho Jumanne kuweka kila kitu bayana.
“Kuna mengi yanasema hadharani na chini ya zuria kuhusu rambirambi, kwa lengo la kuweka bayana kila kitu, tumepanga kukutana na waandishi wa Habari Jumanne (kesho) kuanzia majira ya saa nne,” alisema

No comments:

Post a Comment