Pages

Pages

Friday, April 13, 2012

Tb JOSHUA ATABIRI KIFO CHA MUIGIZAJI NOLLYWOOD

 Baada ya kutabiri kifo cha mmoja wa rais wa bara la Afrika, mtumishi wa Mungu Nabii na Mtume TB Joshua ametabiri kifo cha mwigizaji mwingine wa kiume wa Nollywood na ameomba ukiwa kama MwafriKa anaomba maombi yako kumwombea mungu amuepushie na kifo else basi mapenzi ya Mungu yatimizwe akasema muigizaji huyo ni wa kiume hivyo sala zaidi zinaombwa kwa waigizaji wafanye maombi ya kufunga na kuomba.
Fafanuzi toka kwa wadadisi wa mambo juu ya tabiri zinazotoka kwa kinywa cha mtumishi huyu wa Mungu zinasema.. Kitu ambacho wengi hawaelewi ni kuwa nabii siyo final say. Mungu ndiye final say. Kinachotokea ni kuwa Mungu anamwonesha nabii kitakachotokea mbeleni. Na wajibu wa nabii ni kuomba rehema za Mungu ili ikiwezekana Mungu aahirishe tukio tarajiwa. Mungu huonesha nabii kwa sababu mbili kwamba akae kwenye nafasi yake aombe au basi watu wajue kama halikuwa jambo linalotolewa unabii. Ndio utasikia anasema kwamba yeye anamwomba Mungu na anaomba watu waombe. Kuwa nabii siyo ujiko ila ni kazi maana utadaiwa. Ni mzigo mzito sana ndio maana tangu zamani hatuwi na manabii wengi kwa wakati moja. Yaani lazima kuna nabii na wana wa manabii kama enzi za Eliya.

No comments:

Post a Comment