LUCY STEPHANO NDIYE MISS MBULU 2012
Hayawi hayawi hatimaye yakawa, hatimaye kitendawili cha nani kuibuka kidedea yaani atakayevikwa umalkia wa wilaya ya Mbulu kikateguliwa jana usiku katika ukumbu wa Kituo cha Jamii (Community Centre) kwa wawakilishi kutoka Haydom kuibuka kidedea kwa kushika nafasi za juu kabisa.
Lucy Stephano ambaye ni Miss Haydom No.2 kiunoni,hakuamini masikio yake pale alipotangazwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi laki tatu (300,000/=) huku Linah Emmanuel ambaye alikuwa Miss Haydom No. 3 akiibuka mshindi wa pili na kuweka kibindoni kitita cha shilingi laki mbili (200,000/=).
No comments:
Post a Comment