Pages

Pages

Friday, May 18, 2012

MAFISANGO KUAGWA LEO CHANG'OMBE

MWILI wa mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Patrick Mutesa Mafisango uliokuwa uagwe kesho kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, sasa utaagwa katika viwanja vya TCC Club Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Makamu mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'.
Mafisango aliyefariki kwa ajali ya gari alfajiri ya leo eneo la Keko-VETA jijini Dar es Salaam, baada ya kuagwa mwili wake utasafirishwa kwenda kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa mazishi.

Nyota huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda, ameichezea Simba kwa msimu mmoja akitokea Azam FC.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,Amin

No comments:

Post a Comment