Pages

Pages

Thursday, May 10, 2012

MTOTO WA MWAKA MMOJA ATOROSHWA NA MWANAMKE WA MFANYABIASHARA

Mwanamke Queen Daniel Chonya (26) anayedaiwa kumtorosha mtoto na kukimbia na kiasi cha shilingi milioni 15 za mumewe
Mtoto anayedaiwa kutoroshwa
Mwanamke mkazi wa mji wa Makambako wilaya ya Njombe mkoa wa Njombe Queen Daniel Chonya (pichana juu) anatafutwa na mume wake mfanyabiashara wa mji wa Makambako Timoth Mbuma kwa tuhuma za kumtorosha mtoto pamoja na kukimbia na kiasi cha fedha kiasi cha shilingi milioni 15.
 Mfanyabiashara huyo Bw Mbuma amesema kuwa mwanamke huyo ametoroka na mtoto wa kiume mwenye mwaka mmoja na miezi mitano anayeitwa Given au Juniour na kuwa mwanamke huyo mkazi wa Malangali wilaya ya Mufindi ambaye ameishi naye kwa miaka minne sasa katika eneo la Mwembetogwa mji wa Makambako.
Ameongeza kuwa kabla ya kutoweka yeye na mkewe huyo hapa kuwa na ugomvi wowote na kuwa machi 19 siku ya jumatatu asubuhi ambapo alimuita dukani kwa ajili ya kutumwa bank ya NBC kupeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 15 .
Baada ya kupewa fedha hizo alikwenda nyumbani na kufungasha baadhi ya vitu kama nguo na vyombo na kutoweka na kuwa mwanamke huyo anasemekana yupo jijini Mwanza ama jijini D'Salaam na kuwa hadi sasa tukio hilo limeripotiwa polisi kwa kumbukumbu namba MKB/RB/709/12 na kuwa kwa yeyote mwenye taarifa anaweza kutumia namba 0752242464 au 0786505524 ama 0655505524 kuwa kubwa hapa anahitaji mtoto na kuwa mtu yeyote mwenye taarifa sahihi alipo mwanamke huyo atazawadiwa donge nono

No comments:

Post a Comment