Pages

Pages

Monday, June 11, 2012

CSTHERINE NDIYE REDDS MISS CHANG'OMBE 2012

Redds Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21, akipunga mkono mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa mshindi wa taji hilo ambapo aliwashinda warembo wengine 13 waliokuwa wakiwania taji la Chang’ombe na tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012.

Redds Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21, (katikati) akipunga mkono mara baada ya kusimikwa rasmi kuwa mshindi wa taji hilo. Kulia ni mmshindi wa pili, Jesca Haule (18) na Mshindi wa tatu Zulfa Bundala. Masumbigana aliwashinda warembo wengine 13 katika shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar es Salaam Juni 10, 2012.
 Tano bora ya Miss Chang’ombe 2012 ambao wote wamepata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012 wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka Kushoto ni Zulfa Bundala (21), Jesca Haule (18), Catherine Masumbigana (21), Miriam Nkisigwa (20) na Flora Kazungu.
 Warembo wakicheza show maalum ya ufunguzi
 Warembo wakipita na mavazi ya ubunifu. Kutoka kulia ni Debora Nyakisinda, Like Abraham na Jesca Haule.
 Ilifika zamu ya waarembo wakupita na vazi la ufukweni mbele ya majaji na wapenzi wa sanaa ya urembo nchini waliokuwapo ukumbini hapo. Kutoka kulia ni Debora Nyakisinda, Like Abraham na Jesca Haule.
 Vazi la ufukwenu, Kutoka kulia ni Restituta Faustiney, Wensley Mabula na Clara Diu.
 Miss Chang'ombe 2012, Catherine Masumbigana alivyojinadi na vazi la ufukweni
 Warembo Flora Mayasa (kulia) Catherine Masumbigana (katikati) na Elizabeth Mushi wakiwinda point na vazi la ufukweni.
 Kila mmoja alirusha kete yake, Latifa Mabewa (kulia) akijinadi na Zulfa Bundala
Mkali wa Bongo Fleva Nassib Abdul 'Diamond' na vijana wake walisindikiza show hiyo kwa kutoa burudani kali jukwaani.
 Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana (Mb) Amos Makala akizungumza jukwaani.
 Waratibu wa shindano hilo kutoka King Promotors wakifuatilia onesho. Kushoto ni Tom Chilala.
 Mgeni Rasmi Amos Makala  (kushoto) akimpongeza Mshindi Miss Chang'ombe, Catherine Masumbigana kwa kutwaa taji hilo. Kulia ni Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe.
 Amos Makala (kushoto) akizungumza na Viongozi Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) na Prashant Patel.
 Wapenzi wa urembo kutoka Chuo Kikuu cha Kampala tawi la Dar es Salaam nao walikuwepo.
 Washiriki wa Miss Ilala 2012 kutoka Kitongoji cha Tabata jijini Dar es Salaam nao hawakukosekana
 Familia ya Miss Tanzania 2011, nayo ilikuwepo ni mama yake na mdogo wake.
 Vimwana wa Kurasini ambao pia wamepata tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012 wakiwa ukumbini kushuhudia wapinzani wao wapya walioingia kushiriki nao.
 Wadau kutoka Kampumi ya NeXus walidhamini shindano hilo na kulifuatilia kwa ukaribu zaidi.
 Vijana wa Mapacha watatu walikuwepo jukwaani na kutoa burudani kali.

No comments:

Post a Comment