Pages

Pages

Monday, June 18, 2012

DIAMOND PLATINUM KUPAMBA MISS DAR INTERCOLLEGE 2012

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kupamba shindano la kumsaka Miss dar Intercollege 2012 linalotarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). 
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema kwamba mbali na Diamond, onyesho hilo pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
 Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaosghiriki  wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya  The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam 
 “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
 Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania. 
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan. 
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.

No comments:

Post a Comment