Pages

Pages

Wednesday, June 6, 2012

MISS DAR INTER COLLEGE KUTAMBULISHWA MAFIAN LOUNGE

Warembo wa Miss Dar InterCollege wakiwamejipanga mbele ya wadau na wadhamini katika uzinduzi wa bendi ya SkyLight iliyofanyika  Mafian Lounge iliyopo Masaki, bendi hiyo inamilikiwa na mmoja wa wadhamini wao Ndege Insurance.

Mratibu wa Shindano la  Miss Dar InterCollege Dina Ismail katika hafla ya kuwatambulisha warembo wa shindano hilo alisema kwamba warembo watakaoshiriki  wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.

Alisema mpaka sasa warembo 15 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamesharipoti kambini.Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus, Jane Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.

Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.

“Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano letu…mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na Clouds Fm.
Mratibu wa Shindano la  Miss Dar InterCollege Dina Ismail akimuelekeza jambo mmoja wa wadau wa urembo huku warembo wakipozi kwa picha.
Shampeni ikifunguliwa kama ishara ya utambulisha wa warembo hao katika hafla ya kuwatambulisha iliyofanyika juzi kwenye klabu ya Mafian lounge jijini Dar es salaam.(FULL SHANGWE)

No comments:

Post a Comment