Pages

Pages

Sunday, August 12, 2012

RASH SPORTSAND ENTERTAINMENT(RSE) KUDHAMINI MISS UTALII 2012

HATIMAYE Shindano la Miss Utalii mwaka 2012 linaloshirikisha Wilaya mbili za Kinondoni na Ilala limepata mdhamini ambaye ni Kampuni ya ‘Rash Sports and Entertainment’ (RSE).
Shindano hilo litafanyika Agosti 14 mwaka huu, kwenye Ukumbi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam ambako litashirikisha warembo 30 kutoka katika wilaya hizo mbili.
 
Akizungumza na Fullshangweblog jijini leo, wakati akimnadi mfadhili huyo, Mkurugezi wa Shindano hilo, Methuselah Magese alisema kujitokeza kwa mfadhili huyo, kutasaidia kuamsha ari ya washiriki kwa kuutangaza vizuri mkoa wa Dar es Salaam kiutalii.
 
Alisema mfadhili huyo, ameahidi kusaidia kipindi cha mazoezi kilichobaki cha wanyange hao, ambako awali mazoezi hayo yalikuwa yakifanyika katika hoteli ya Traventine na hivi sasa kuhamia Lamada.
 
“Lengo la shindano hili ni kutaka kuligeuza jiji la Dar es Salaam kuwa kivutio cha utalii kama ilivyo kwa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha”alisema Magese.
 
Akizungumzia maandalizi kuhusu warembo hao, Magese, alisema warembo wote 30 wanafanya mazoezi kwa juhudi pia wako vizuri kiakili katika kuchambua mada mbalimbali walizojiandalia kwa ajili ya siku fainali.
 
Naye Mkurugenzi wa RSE, Rashid Mrisho, alisema kwa kuwa biashara nyingi zimekuwa zikiendelea kupitia matangazo, hivyo kuwasaidia warembo hao ni moja ya fursa itakayoleta chachu katika  kuvitangaza viashiria vyote vya utalii vilivyoko katika jiji hilo.

No comments:

Post a Comment