Pages

Pages

Monday, August 27, 2012

Warembo Redds Miss Kanda ya mashsriki kuingia kambini leo

Miss Morogoro 2012 Joyce Baluhi katikati akiwa na washindi wenzake, Salvina Kibona mshindi wa pili kushoto na Irene Thomas mshindi wa tatu. Warembo hawa ni miomngoni mwa wanaoingia Kamoni hii leo.
*******
JUMLA ya warembo 14 wanaotaraji kuwania taji la Miss Redd's Kanda ya Mashariki 2012 Wanataraji kuiongia kambini mjini Morogoro jioni ya leo tayari kwa maandalizi ya shindano hilo.
Shindano la Redds Miss Kanda ya Mashariki 2012 linataraji kufanyika Septemba 1, 2012 katika Hoteli ya Kisasa ya Nashera iliyopo mjini Morogoro.
Aidha wanyange hao walichelewa kunza kambi yao kupisha warembo hao kuhesabiwa makwao kabla ya kuingia kambini.
Akizungumza na Father Kidevu Blog, mratibu wa shindano hilo Alexander Nikitas alisema warembo hao pia walishiriki kuhamasisha zoezi la sensa katika maeneo mbalimbali wanayotoka Huku wale wa Mkoa wa Morogoro wakihamasisha mjini hapo watu kushiriki kuhesabiwa.
Kanda ya Mashariki inaundwa mna mikoa mine katika shindano hilo dogo la Miss Tanzania 2012 ambayo ni mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani.
Nikitas aliwataja washiriki watakao ripoti kambini katika Lodge ya Usambara Safari Resort iliyopo nane nan mkoani Morogoro kuwa ni Zuhura Gora,Alice Adam na Shakila Hassan kutoka Mtwara.
Wengine mikoa yao kwenye mabano ni Maria Peter,Irene Mweleko na Rose Lucas(Pwani) Irene Veda,Stella Bartazary na Darina Athumani(Lindi) na kutoka Morogoro ni pamoja na Salvana Kibano,Joyce George,Irene Thomas,Betina Msofe,na Nafia waziri.
Taji la Miss Kanda ya Mashariki linashikiliwa na Loveness Flavian ambaye pia ni Miss Sport Woman wa Miss Tanzania 2011. Warembo hao watakuwa chini ya Mwalimu Asha Salehe Miss Eastern Zone namba tatu. 
Kwa mujibu wa Nikitas wadhamini wa shindano hilo Mbunge wa Kilosa Mustafa Mkulo,Redd's, Dodoma wine, Father Kidevu Blog, Auckland Travel Safairi Tour, Clouds Fm, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, Endepa Event Planner, Jambo Leo, Kitwe General Traders na Simple Easy Car Renta

No comments:

Post a Comment