Pages

Pages

Friday, September 28, 2012

Tanzania kutangaza mshiriki wa Miss East Africa Oktoba 14


 
Mrembo atakaeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya mwaka huu ya urembo ya Miss East Africa atatangazwa rasmi tarehe 14/10/2012 katika hotel ya Serena Jijini Dar es salaam.

Jumla ya warembo 148 wameomba kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss East Africa mwaka huu lakini ni Mrembo mmoja tu atakaechaguliwa kuiwakilisha Nchi katika mashindano hayo makubwa ya urembo katika ukanda huu wa Africa na yanayosubiliwa kwa hamu na wapenzi wa fani hiyo ndani na Nje ya Africa Mashariki 

Aidha maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri ambapo yatafanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam

Wakati huohuo Nchi ya Burundi imebadili mwakilishi wake ambapo sasa itawakilishwa na mrembo Ariella Kaneza (23), Mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo kikuu cha Universte De Lumiere akichukua Degree ya marketing.

Taarifa kutoka Burundi iliyosainiwa na Mratibu wa Mashindano ya Miss East Africa Nchini humo, Serge Nkurunziza, zimeeleza kwamba Burundi imeamua kubadili mwakilishi wake ili kuhakikisha kwamba Nchi hiyo inashinda Taji hilo kwa mara ya pili tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1996 baada ya kugundua kwamba mwakilishi wake wa awali anapungukiwa baadhi ya sifa chache za kuweza kunyakua taji hilo. (Burundi imewahi kushinda Taji hilo mara moja mwaka 2008 kupitia kwa mrembo wake Miss Claudia Niyonzima)
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake na yatashirikisha warembo kutoka Nchi 16 za ukanda wa Afrika Mashariki.

Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika.

Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.

Thursday, September 27, 2012

MAMA AFRIKA SARAKASI YAFANA

... ilikuwa ni maajabu na kweli.
 
Kijana mwingine alionyesha umahili wake ni huyu kama vile unavyomuona.
Michezo ya kamba nayo ilikuwa ya kuvutia.
 Mchezo mwingine ulikuwa niwa kurushiana vikapu ya kutimia miguu.
 Vijana wakionyesha uhodari wao wa kupaa juu.
 
Vijana wakiaga mara baada ya onyesho kumalizika.

Tuesday, September 25, 2012

MISS TANZANIA 2012 YAPAMBA MOTO, HAWA NDO WAREMBO WATAKAOSHIRIKI MISS TANZANIA

Redds Miss Lake zone 2012/13 Eugene Fabian (katikati) akiwa pamoja na , mshindi wa Tatu Happiness Rweyemamu na Kulia kwake ni mshindi wa pili Happiness Daniel warembo hawa wataingia kambi ya REDDS Miss Tanzania 2012.

Redds Miss kanda ya Kaskazini Warida Frenk katikati akiwa na washindi wenzake Anande Raziel kulia na lucy stefano kushoto mara baada ya kutawazwa kuwa washindi wa Redds Miss Kanda ya kaskazini,Washindi hao wanatarajiwa kujiunga kwenye kambi ya Redds Miss Tanzania hapo baadae ili kujiandaa na shindano la Taifa la Redds Miss Tanzania.

Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas katikati akipunga mkono kwa furaha akiwa na mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa tatu Joyce Baluhi mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa Septemba Septemba 1, mwaka huu. Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.

Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana George Hussein na mshindi watatu Irene David. Brigit pia anashikilia taji la Redds Miss Sinza 2012 huku Irine akishikilia taji la Miss Ubungo 2012.

Malkia wa Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester (katikati), akiwa na mshindi wa pili Flavian Maeda (kushoto), pamoja na Catherine Masumbigana aliyeshika nafasi ya tatu katika kilele cha mashindano hayo, Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

 Naomi Jones, Caren Elias na Venance Edward


Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo (katikati) akiwa na mshindi wa pili Lightness Michael (kushoto) na mrembo aliyetwaa nafasi ya tatu Elizabeth Diamond baada ya kumalizika kwa shindano hilo mjini Dodoma hivi karibuni. warembo hawa wote wameingia kambi ya Miss Tanzania 2012.


Redds Miss Ilala 2012, Noela Michael akiwa na mshindi wa pili Magdalena Munisi (kulia) na mshindi wa tatu Mary Chizi (kushoto) mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Ilala 2012.
Jumla ya warembo 30 wanataraji kuingia kambi ya REDDS MISS TANZANIA 2012 wakati wowote baada ya kumalizika kwa mashindano ya Vitongoji, Mikoa, na hatimaye Kanda mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa mashindano hayo ya Kanda ambayo kila Kanda imetoa washindi wa tatu ambao wataziwakilisha Kanda zaoi katika Shindano hilo kubwa na laiana yake.
Warembo hao na Kanda zao wanazotoka ni Redds Miss Kanda ya Kaskazini Warida Frenk, Anande Raziel na Lucy Stefano, Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012 ni  Rose Lucas, Irine Veda na Joyce Baluhi , Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, Diana George Hussein na Irene David.
Kanda nyingine ni Redds Miss Lake zone 2012 Eugene Fabian,Happiness Daniel na Happiness Rweyemamu, Redd's Miss Tameke 2012, Edda Sylvester, Flavian Maeda na Catherine Masumbigana, Redds Miss Kanda ya Kati, Belinda Mbogo, Lightness Michael na Elizabeth Diamond.
Washiriki wengine watakao ingia Kambini ni kutoka kanda ya Redds Miss Ilala 2012, Mary Chizi, Magdalena Munisi na Noela Michael, Redds Kanda Vyuo vya Elimu ya Juu, Virginia Mokiri, Fatma Ramadhani na Fina Revocatus, kanda nyingine ni ya Kutoka Chuo Kikuu Huria ni Zuwena Nassibu na Redds Miss Southern Zone Naomi Jones, Caren Elias na Venance Edward.
Kesho Septemba 26, 2012 Kamati ya Miss Tanzaniaikiongozwa na Mkurugenzi wake Hashim Lundenga kutoka Lino International Agency watakutana na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maeleo majira ya saa 4:00 asubuhi kuzungumzia maandalizi ya Kambi hiyo

DIAMOND NA WACHUMBA 30...LINAH,RECHEL KIMIANI


Wanamuziki wa bongo flava wakiwa katika picha ya pamoja siku ambapo walikuwa mbeya katika show ya Fiesta mjini mbeya,Diamond akiwa amezishilia the nidoz of wasanii wenzake Lina(kulia) na  upande wakulia(recho) ndo inasemekana msababisho huenda ukaangukia huko,kitu ambacho kimetafsiriwa Diamond ana pepo la ngono dhidi ya watu maarufu.

Monday, September 24, 2012

EDDA SYLIVESTER NDIYE MISS TEMEKE 2012

Redd's Miss Temeke 2012, Edda Sylivester (katikati) akipunga mkono kwa furaha akiwa na washindi wenzake mshindi wa pili Catherine Masumbigana (kushoto) na Flaviana Maeda (kulia) mara baada ya kutangazwa washindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam.

Friday, September 21, 2012

FLAVIAN MATATA AOSHA NYOTA LONDON FASHION WEEK

Mwanamitindo Flaviana Matata kutoka Tanzania , akipita jukwaani wakati wa Onyesho la wiki ya  mitindo, jijini London, jana.

Thursday, September 20, 2012

MIMBA YA AMBER ROSE NJE NJE..!


 Amber rose hivi mapema ametupia picha kwenye mtandao wa twitter ikionesha ujauzito wake aliopewa na mchumba wake Wiz khalifah
Amber ambae alikuwa katupia chupi ya pinki iliofunika tatoo yake kwa chati na kiblauzi kilichoyabili matiti yake  kwa nadranadra ,, amber ameonekana mwenye furaha sana baada ya kupata ujauzito huo ambao umemuweka karibu zaidi na mchumba wake  Wiz. 

JAY-Z&BEYONCE WAMWAGIA MANOTI RAIS OBAMA


With Beyonce on his side, there’s pretty much no way President Obama can lose.

Jay-Z and Beyonce played host to a lavish fundraiser at Jay’s 40/40 club in New York City for President Obama, which reportedly raised $4 million dollars and cost donors $40,000 per plate.
And unlike when he knocked his other famous hip hop supporter Kanye West on the head for being rude to Taylor Swift, Obama did everything he could to link himself to hip hop’s classiest and richest power couple.
The L.A. Times reports that the president noted that he and Jay-Z have one thing in common.
“We both have daughters and our wives are more popular than we are. So, you know, we’ve got a little bond there. It’s hard but it’s OK,” said Obama.
The president also praised Beyonce as a role model for his daughters.
“Beyonce could not be a better role model for my girls,” Obama said.
Now wait a minute. Beyonce is certainly one of the better behaved pop stars of her generation, but does the president mean that Sasha and Malia should look up to Beyonce for her mean pelvic thrust game?

AFARIKI KWA KUONGEZA UKUBWA WA SEHEMU ZA SIRI


 Ni  Stori ya kusikitisha, inatokea nchini Marekani ambako kijana Justin Street, amepoteza maisha akiwa kwenye jaribio la kuongeza ukubwa wa nyeti yake.
Habari kamili ipo hivi; Justin, 22, akiwa baba wa watoto wawili alikwenda kwa mwanamama Kasia Rivera ,35, aliyejitangaza kuwa ni mtaalamu wa tiba za kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume.
Kasia aliweka matangazo barabarani kuwa anayo tiba ya kuongeza ukubwa wa nyeti za kiume, hivyo kumfanya Justin ahamasike kwenda kupata dawa hiyo ili kujiongezea ushababi.
Wanasema tamaa mbele mauti nyuma, ndivyo ilivyotokea kwa Justin, kwani baada ya kuomba dawa ya kuongeza ukubwa wa maumbile yake ya kiume, alidungwa sindano yenye madini ya silikoni.
Madini hayo, alidungwa kwenye nyeti yenyewe na baada ya muda mfupi, hali ya afya yake ilibadilika kuwa mbaya, alizorota na siku iliyofuata alifariki dunia.
Kutokana na tatizo hilo, Kasia alifikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji akituhumiwa kufungua zahanati bubu ndani ya nyumba yake iliyopo New Jersey, vilevile kutoa tiba za kiafya wakati hana taaluma hiyo wala leseni ya kuendesha kazi hiyo ya utoaji huduma za afya.
Kasia alipandishwa kizimbani wiki iliyopita, uchunguzi wa maiti umethibitisha kwamba Justin alifikwa na mauti baada ya madini ya silikoni aliyodungwa kwa sindano kuziba njia za mishipa ya damu.
Mmoja wa madaktari waliomfanyia uchunguzi Justin alisema kuwa hii ni mara ya kwanza kusikia silikoni inayotumika kuongeza ukubwa wa matiti ya wanawake imetumika kwenye kuongeza ukubwa wa uume.Kasia, amekana kuhusika na mauaji hayo.

AUNT EZEKIEL NA NISHA WANAELEKEA KUCHAPANA MAKONDE

BAADA ya msanii wa filamu Salma Jabu ‘Nisha’, kulitaka  ’BASATA’  k u mchukulia hatua kali msanii Aunty Ezekiel kwa madai p icha zake za nusu utupu zinachafua maadili na kuwafanya wasanii wote waonekane wahuni, naye amekuja juu na kumtaka Nisha afanye mambo yake na aache tabia ya kumfuatilia.

Hata hivyo baada ya kutokea ishu ya Ezekiel bado wasanii wanaendelea kukumbwa na skendo chafu kwani naye Wema Sepetu kuna baadhi ya picha mitandaoni zinamuonesha sehemu kubwa makalio yake yakiwa wazi kitu ambacho kinaendelea kuwamaliza bongo movie.

Ezekiel alidai kuwa haoni sababu ya Nisha, kumtolea maneno hayo kwani hata yeye ana matatizo yake hivyo anatakiwa kujichunguza yeye ndipo aende kwa mtu mwingine.

Alidai kwa sasa anatumia lugha ya kistaarabu zaidi yani haitaji bifu lakini akizidi kumfuatilia atachanua makucha, ingawa hana tabia ya kuchukuiana na mtu ila kwa hili hajakubaliana nalo kwani wapo wasanii wagapi wanakosea na hajawahi kutoa kauli kama hiyo.

Hata hivyo aliongeza kuwa asitake kutumia kauli za mpenzi wake Ney, kuwa makahaba wako bongo movie kwani hata mwenyewe ni mmoja wa wasanii wa tasnia hiyo.

DIANA MAINANSON UNIQUE MODEL NAMBA 2 ANAETESA NCHINI MALYASIA

 Diana Mainanson mshindi namba 2 Unique Model 2010 ambae nidie atakuwa  mmwalimu wa catwalk katika Unique Model season II,Diana kwa sasa yuko nchini Malyasia ambapo mwezi wa kumi atarudi Dar kwaajili ya kuwafundisha models wapya ambao watakaochaguliwa katika Unique Model   season II katika kumtafuta Unique model of the year 2012
 

Tuesday, September 18, 2012

WARDA FRANK ALIVYOIBUKA MISS KANDA YA KASKAZINI 2012

Redds Miss kanda ya Kaskazini Warida Frank katikati akiwa na washindi wenzake Anande Raziel kulia na lucy stefano kushoto mara baada ya kutawazwa kuwa washindi wa Redds Miss Kanda ya kaskazini,Washindi hao wanatarajiwa kujiunga kwenye kambi ya Redds Miss Tanzania hapo baadae ili kujiandaa na shindano la Taifa la Redds Miss Tanzania
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora kwenye shindano la Redds Miss kanda ya Kaskazini wakiwa katika Picha ya pamoja kabla ya kutangazwa kwa washindi waliofanikiwa kushika nafasi tatu za juu ambapo Washindi hao wanatarajiwa kujiunga kwenye kambi ya Redds Miss Tanzania hapo baadae ili kujiandaa na shindano la Taifa la Redds Miss Tanzania.

MISS TEMEKE 2012 KINDUMBWENDUMBWE..!!



Kamati ya  Miss Tanzania  inatarajiwa kutembelea kambi ya Temeke 2012, kubwa ni kuwafunda vimwana hao kutoka Vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe, kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mashindano ya urembo.

Kamati hiyo itaongozwa na Mkurugenzi wake, Hashim Lundenga atakayefuatana na mshauri wa masuala ya urembo katika kamati yao, Dk. Ramesh Shah, katibu Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye na mjumbe wa kamati hiyo, Lucas Rutta.

Shindano la   Miss Temeke 2012, linafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa PTA (SabaSaba Hall) na tiketi za VIP zimeshaanza kuuzwa katika Club za City Sports Lounge iliyopo makutano ya Samora na Azikiwe na Nyumbani Lounge iliyopo maeneo ya Namanga ambapo VIP kwa mtu mmoja ni Tshs 50,000 na pia waweza nunua kwa meza moja ama ya watu 8 kwa laki 4 au watu kumi laki 5.

Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda, Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

Shindano hili litakuwa ni miongoni mwa mashindano ya lala salama kabla ya kupata warembo watakaoungana na warembo wa kanda nyingine kuingia kambini kumtafuta mrembo wa Redds Miss Tanzania kwa Mwaka huu.

Monday, September 17, 2012

SALOME KIULA NA FATMA HUSSEIN WAIBUKA WASHINDI MISS UTALII

 
 Miss Utalii Wilaya ya Ilala, Salome Kiula (katikati) akiwa amepozi pamoja na mshindi namba mbili Caroline Yust (kulia) na mshindi wa tatu Lucy Julius.
 Miss Utalii Wilaya ya Ilala, Salome Kiula (kulia) akiwa na Miss Utalii Wilaya ya Kinondoni Fatuma Hussein muda mfupi baada ya kutawazwa kuwa mamalikia wa utalii katika mashindano yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

 Miss Utalii mwenye kipaji Wilaya ya Ilala, Zourha Malisa
 Miss Utalii mwenye kipaji Wilaya ya Kinondoni, Doreen Pereus 
 
 
 
 
 Mkurugenzi wa duka la uuzaji wa nguo za ndani za wanawake la Secret Lengerie, ambao ni wadhamini wa mashindano hayo, Fatna Tambwe akizungumza na umati wa watu waliofurika kushuhudia mashindano hayo.
 Mkurugenzi wa duka la uuzaji wa nguo za ndani za wanawake la Secret Lengerie, ambao ni wadhamini wa mashindano hayo, Fatna Tambwe
 
 
 Mkurugenzi wa duka la uuzaji wa nguo za ndani za wanawake la Secret Lengerie, ambao ni wadhamini wa mashindano hayo, Fatna Tambwe akitoa zawadi kwa miss utalii kiaji, Zourha Malisa
 
 

 Mkurugenzi wa duka la uuzaji wa nguo za ndani za wanawake la Secret Lengerie, ambao ni wadhamini wa mashindano hayo, Fatna Tambwe katika picha ya pamoja na mamiss utalii Ilala na Kinondoni