Pages

Pages

Thursday, September 20, 2012

AUNT EZEKIEL NA NISHA WANAELEKEA KUCHAPANA MAKONDE

BAADA ya msanii wa filamu Salma Jabu ‘Nisha’, kulitaka  ’BASATA’  k u mchukulia hatua kali msanii Aunty Ezekiel kwa madai p icha zake za nusu utupu zinachafua maadili na kuwafanya wasanii wote waonekane wahuni, naye amekuja juu na kumtaka Nisha afanye mambo yake na aache tabia ya kumfuatilia.

Hata hivyo baada ya kutokea ishu ya Ezekiel bado wasanii wanaendelea kukumbwa na skendo chafu kwani naye Wema Sepetu kuna baadhi ya picha mitandaoni zinamuonesha sehemu kubwa makalio yake yakiwa wazi kitu ambacho kinaendelea kuwamaliza bongo movie.

Ezekiel alidai kuwa haoni sababu ya Nisha, kumtolea maneno hayo kwani hata yeye ana matatizo yake hivyo anatakiwa kujichunguza yeye ndipo aende kwa mtu mwingine.

Alidai kwa sasa anatumia lugha ya kistaarabu zaidi yani haitaji bifu lakini akizidi kumfuatilia atachanua makucha, ingawa hana tabia ya kuchukuiana na mtu ila kwa hili hajakubaliana nalo kwani wapo wasanii wagapi wanakosea na hajawahi kutoa kauli kama hiyo.

Hata hivyo aliongeza kuwa asitake kutumia kauli za mpenzi wake Ney, kuwa makahaba wako bongo movie kwani hata mwenyewe ni mmoja wa wasanii wa tasnia hiyo.

No comments:

Post a Comment