Pages

Pages

Friday, September 14, 2012

IRENE UWOYA: JACKLINE WOLPER HANA KIWANGO CHA KUCHEZA FILAMU YANGU

MSANII anayeshikilia soko la filamu kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza scenes za mapenzi na hata zile za kijamii, Irene Uwoya, amedai mashabiki wake wengi wanamtaka acheze filamu moja na hasimu wake mkubwa Jackline Wolper, ila moyo wake haupo tayari kwani anaamini msanii huyo kiwango chake ni kidogo hivyo kwenye filamu anaweza kumtia hasara ya sokoni.

Mwandishi wahabari hii  alipotaka kujua ni lini watakuja kushiriki filamu ya pamoja ili kuwaonesha mashabiki wao viwango vyao, ndipo alipoamua kutoa kauli hiyo kuwa kiwango chake ni kikubwa na hakuna asiyejua hilo hivyo akishiriki kazi moja msanii huyo wote wanaweza kuonekana chipukizi kwani filamu inaweza kuwa mbaya kuliko maelezo.

“Nadahani unajua mimi na huyo msanii tukoje hivyo sidhani kama naweza kushiriki kwenye filamu yake au yangu kwa sababu najua kiwango chake ni kidogo mno, ingawa sisemi kwamba hajui kuigiza ila bado hajafikia mziki huu,” alidai Uwoya.

Hata hivyo Wolper alipotafutwa ili kuongelea kiwango anachosema Uwoya hakuweza kupatikana na hadi kazi hii inaenda mitamboni simu yake ilikuwa haipatikani.

No comments:

Post a Comment