Pages

Pages

Friday, September 7, 2012

MISS ILALA 2012 KUJULIKANA LEO


MEYA wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kinyang’anyiro cha kumsaka Redd’s Miss Ilala 2012 kitakafanyika leo kwenye ukumbi wa Nyumbani Lounge Namanga jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Redd’s Miss Ilala 2012, Juma Mabakila, alisemba  Miss Ilala mwaka huu, atazawadiwa  sh milioni 1.5, mshindi wa pili sh mil 1.2 wa tatu sh 700,000 wa
nne na wa tano watapatia sh 400,000 kila mmoja huku waliobakia watapata kifuta jasho cha sh 200,000.
Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa msabnii nguli wa kizazi kimpya nchini Lady Jaydee na Machozi Band, Banana, Ommy Dimpoz na Chege.
Warembo watakaopanda jukwaani leo kumrithi Salha Israel ambaye pia ni Miss Tanzania, ni Mary Chizi, Matilda Martin, Mgdalena Munisi na Suzan Deodatus.
Aliwataja warembo watakaowania taji hilo ni pamoja na Whitness Michael, Stella Moris, Elizabeth Perty, Wilmina Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Saidi, Diana Simon,Amina Sangwe, Noela Michael na Phillios Lemi.

No comments:

Post a Comment