KUMEKUCHA MISS TANZANIA VIPAJI @ GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL
Shindano la kumsaka mnyange mwenye kipaji Miss Tanzania litafanyika tarehe 26 kuanzia saa moja usiku mwezi huu octoba katika hoteli ya Giraffe ocean view iliyoko mbezi beach.
Kiingilio ni 15,000/= kama utanunua tiketi kabla ya siku ya tukio ambapo tiketi hizo zinapatikana Shear Illussion ya mlimani city na 20,000/= ukilipa mlangoni.
Burudani tosha toka kwa warembo hao itatolewa pia wasanii mbalimbali watatumbuiza siku hiyo,karibu ushuhudie vipaji vya warembo wa Tanzania katika hoteli yenye madhali tulivu na ya kuvutia Giraffe ocean view.
No comments:
Post a Comment