Pages

Pages

Monday, October 15, 2012

NEY WA MITEGO AWASHAMBULIA UPYA BONGO MOVIE


BAADA ya ngoma yake ya ‘Nasema Nao’, kuleta misusuko kibao ndani ya tasnia ya filamu bongo kiasi cha kutishiwa maisha sasa msanii Ney Wa Mitego ameamua kutoa majibu kwa watu waliodhani kuwa hatoweza kuendelea kuwapa ukweli wao wasanii wa bongo movie, ambapo sasa pini lake jipya la ‘Wamenichokoza’, ni zaidi ya ‘Nasema Nao’ kwani ujumbe wake mzito.

Msanii huyo ameweza kufikisha ujumbe kwa wasanii wa bongo movie hasa wanawake ambao wanaishi kwa kutengemea wanaume, huku wakisahau kuwa wao ni kioo cha jamii wanatakiwa kuishi maisha ambayo ni mfano kwa wengine.

Akizungumza  msanii huyo alisema kuwa ngoma hiyo kimewajibu wale wote waliodhani kuwa hatoweza kuleta mashambulizi mengine, kwani baada ya ngoma yake ya ‘Nasema Nao’ alipokea simu nyingi za vitisho kutoka kwa watu mbalimbali.

Msanii huyo alidai kuwa kufanya kwake muziki hakumanishi kwamba anatafuta bifu na mtu, kwani anafanya kwa lengo la kuburudisha na kufundisha jamii hivyo kila kitu ambacho anakuwa anakiimba ni mawazo yake lakini anachukizwa na watu wanaomtishia maisha, kamwe hawatoweza kumziba mdomo.

“Hakuna mtu anayeweza kuniziba mdomo na ndiyo maana kazi zangu zinakuwa na ukweli siku zote, na ndani ya ngoma hii mpya utaona vitu vilivyochambuliwa na kufanyiwa uchunguzi wa kina, mbona watajuta mwaka huu,” alisema Ney.

No comments:

Post a Comment