Pages

Pages

Friday, October 12, 2012

OMMY DIMPOZ ADAIWA KUMNYATIA SHILOLE

INASEMEKANA kuwa kimwana anayetesa kwenye filamu na muziki Shilole na Ommy Dimpoz, wapo katika mahusiano ya chini chini na hawataki kuyaweka wazi kwa kuogopa midomo ya watu.

Chanzo kilicho karibu na msanii Shilole kilitoa fununu ya ishu hiyo kwa kudai kuwa wasanii hao mara nyingi wamekuwa wakikutana nyakati za usiku na awali kabisa walikuwa kama marafiki lakini kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ukaribu wao uliongezeka na kuanzisha mahusiano.

Mdaku huyo alidai kuwa hakuna mtu anayejua wasanii hao kama wana mahusiano, kwani wanafanya siri kwa kuogopa vyombo vya habari na hata wanapotaka kuonana huwa wanatumia usafiri wa kukodi kwa sababu tayari magari yao yanajulikana.

“Ishu ambayo mimi naijua ndiyo hiyo kwa sababu ukaribu wao umekuwa mkubwa na sijui kama wanaweza kusema si wapenzi, kuna sehemu tata ambazo nimewahi kuwakuta na wakaniambia nisitoe ishu hiyo kwa mtu yeyote,” kilidai chanzo hicho.

Hata hivyo chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kudai kuwa zipo tabia ambazo mara nyingi Shilole amekuwa akizifanya, kama za kutoka usiku lakini sasa hana ishu hizo na inadaiwa kuwa Dimpoz ndiyo aliyemshauri na kumsihi atuliye na kama wanataka kutoka basi lazima wawe wote.

Shilole alidai kuwa yupo Morogoro kikazi lakini kuhusu kutoka na Dimpoz alikana kwa madai wao ni marafiki na huwa wanakutana kwenye kazi tu.

Aliongeza kuwa yeye anatoka na msanii mwingine kabisa ambaye mara zote watu wamekuwa wakimuona nae.

“Sina mahusiano ya kimapenzi na Dimpoz na huyo mtu anayetaka kuzungumzia ishu ambayo haipo anamatatizo yake, Dimpoz ni rafiki yangu sana tena kwa sababu ni msanii mwenzangu na hakuna kikubwa ambacho kinaendelea kati yetu,” alisema Shilole.

No comments:

Post a Comment