Pages

Pages

Thursday, October 25, 2012

SHILOLE NAE AZIANIKA NGUO ZAKE ZA NDANI JUKWAANI


KATIKA kile kilichoonekana kama wasanii wa Bongo Movies wana ‘aleji’ na kujisitiri miili yao, baada ya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel, safari hii Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameanika sehemu zake za siri kweupe.

Mpaka sasa tuna picha zinazomwonesha Shilole ambaye kwa sasa amegeukia muziki wa mduara, akiwa jukwaani huku akionekana hana habari kabisa na kitu kinachoitwa staha achilia mbali heshima.

Chanzo chetu cha habari kwa sharti la kutotajwa jina lake , kilinyetisha kwamba, Shilole amekuwa na kawaida ya kujiachia kihasarahasara hasa anapokuwa kwenye shoo na bendi yake.

Mdau wa filamu Jumanne Athuman, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam, alisema amekerwa sana na kitendo cha Shilole kukaa hovyo jukwaani kwani anajidhalilisha mbele ya jamii ambayo itajitizama kupitia kwake.

“Huyu Shilole hana heshima kabisa, juzi tu nilisoma katika mitandao akiwakashfu Wema na Aunt eti ndiyo tatizo Bongo Movies, mbona naye huwa anajiachia hovyo?

“Kwa nini hawa wasanii hawajiheshimu? Inaniuma sana, nahisi kama ndiyo kawaida yao. Ni sikio la kufa…hawasikii dawa. Wamezidi sana, wanajichafulia heshima zao kwenye jamii,” alisema Jumanne.

No comments:

Post a Comment