Pages

Pages

Thursday, November 29, 2012

VIBAKA WALIIBA VITU VYA SHARO MILIONEA BAADA YA AJALI KUTOKEA


 Kitendo cha baadhi ya wananchi wa kijiji ilipotokea ajali ya sharo milionea kumwibia 
 kila kilichowezekana kubebeka kimelaaniwa na watanzania waungwana.
 Kumbukeni Sharo ni mtanzania mwezetu,ndugu yetu na msanii wetu mlitakiwa kuwa na utu na sio kukimbilia kuiba vitu vya thamani bila kujali thamani ya mtu.
 Marehemu sharo milionea alikutwa na singilendi na boxa tu vitu vingine kama siumu,cheni,nguo,wallet, redio ya gari ,n.k havikupatikana kutokana na watu kugeuza ajali ya msanii huyo kuwa mtaji kwa watu hao wenye tamaa kuliko utu.
 Blog hii ya jamii inakemea vitendo hivyo vya kupora mali za ndugu zetu pindi wanapopata ajali,wanapaswa kutoa msaada na sio kuona ndiyo muda wa neema kuchukua vitu vya wajeruhiwa au marehemu.

No comments:

Post a Comment