Pages

Pages

Friday, December 14, 2012

CHAZ BABA NA MASHUJAA BAND KUWASHA MOTO FAINALI ZA UNIQUE MODEL DESEMBA 28


Bendi ya ya mziki wa dansi Mashujaa iliyo narappa mahili Chaz Baba inatarajiwa kutoa burudani ya aina yake siku ya ijumaa tarehe 28 mwezi huukatika  fainali za kumsaka mshindi wa shindano la Unique model 2012.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi mratibu wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesibitisha kuwepo kwa bendi hiyo yenye maskani yake jijini dar ndani ya ukumbi wa New maisha club.

 Wapenzi na wadau wa mitindo wajitokeze kuja kushuhudia kinyang'anyiro hiko siku hiyo kwani kina mvuto wa aina yake kwakua maandalizi ya shindano hili yamepangiliwa na kupangika kuanzia burudani ya caltwak toka kwa wanamitindo haompaka burudani ya muziki.

 Jumla ya wanamitindo 12 watapanda jukwaani siku hiyo kuwania taji hilo la Unique model of the year 2012,aidha kutakuwa na na vitu vizuri vya kustukiza 9suprize) kwa wapenzi wa unique model watakaokuwa wamejitokeza siku hiyo ya tarehe 28.

 Shindano hili limedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Kitwe general Traders,sophanaa investment ltd,dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania Daima,Gazeti la Kiu,mashujaa investment ltd,Michuzi blog,jiachie blog,mtaa kwa mtaa blog,Fabak fashins,Genessis health center na Yung don Records.

No comments:

Post a Comment