Pages

Pages

Thursday, December 13, 2012

MSHINDI WA TAJI LA UNIQUE MODEL KUPATIKANA DESEMBA 28

Fainali za kumsaka Unique model of the year 2012 katika shindano la Unique model zitafanyika katika tarehe 28 desemba mwaka huu katika ukumbi wa New Maisha club uliopo Oyterbay jijini Dar.

Fainali hizi zitasindikizwa na burudani ya toka bendi ya Mashujaa ikiongozwa na Chaz Baba,mfalme Costa Siboka atatoa burudani ya vionjo vya nyimbo za asili na upande wa bongo flava kutakuwa na suprize yakufa mtu,pia kwa mara kwanza jukwaani msanii Bshop atapiga bonge la shoo. 

 Wapenzi wa burudani na tasnia ya mitindo wameombwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani atavishwa taji hilo ambalo limekua gumzo jijini Dar kutokana na ushindani mkubwa kati ya washiki hao 12.

Baada ya shindan kumalizika burudani ya wasanii kibao wa bongo flava itaendelea mpaka alfajiri kwani tumepania kukonga nyoyo za mashabiki wa burudani siku hiyo ambapo uhondo huowote  utakuwa ni kwa Tsh 15,000/= tu.

Red carpet kwa mastaa na watu wote watakaopendeza siku hiyo itakuepo,pia kutakua na kitu kipya kabisa katika matukio ya mitindo nchini Tnzania.

No comments:

Post a Comment