Pages

Pages

Tuesday, January 15, 2013

ASHUSHIWA KICHAPO BAADA KUDAIWA NDIYE MBAKAJI WA WATOTO

Mwananchi huyu mwenye hasira kali akimnyanyua juu kibaka huyo na kumtupa chini kama akina 'John Cena'.
..Kichapo kikiendelea kwa kibaka huyo.
Kibaka huyo akizidi kuhukumiwa mtaani.
Ustadhi akijaribu kumnusuru kibaka huyo.
Ustadhi huyo aliamua kuondoka na kibaka ili kumwokoa.
Akimpeleka kituo kikuu cha polisi kilichopo jirani na eneo hilo la Shani.
KIJANA mmoja anayesadikiwa kuwa ni kibaka mchana huu amenusurika kifo baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananachi wenye hasira wakimshutumu kuiba watoto wadogo na kwenda nao eneo la mto Morogoro chini ya daraja la Shani na kuwafanyia vitendo vya kihuni.
Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Athuman alidai kwamba kijana huyo ana kawaida ya kuwateka watoto wadogo hasa wa shule na kuwapeleka chini ya daraja hilo na kuwafanyia vitendo vya kihuni.
" Kwa kipindi kirefu tulikuwa tukimsaka kibaka huyu ambaye ana tabia ya kuwateka watoto wadogo na kuwapeleka mto wa Morogoro chini ya daraja la Shani.
"Muda huu tumemfuma akiwa chini ya daraja hilo na mtoto mdogo ndipo tulipomfukuza na kufanikiwa kumkamata eneo hili la kituo cha mafuta jirani na daraja hili la Shani," alisema Juma Athuman.
Katika hatua nyingine 'ustadhi' mmoja alijitosa na kumnyakua kibaka huyo kutoka mikononi mwa kundi la wananchi hao na kumpeleka kituo kikuu cha polisi kilichopo jirani na eneo hilo la Shani.

No comments:

Post a Comment