Pages

Pages

Thursday, January 17, 2013

INASIKITISHA ...KICHANGA CHATUPWA KANDO YA CHUO CHA TUMAINI

Mtoto wa jinsia ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja amekutwa ametelekezwa pembeni ya mto karibu na chuo kikuu cha Tumaini Iringa.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa kitendo hicho ni cha kinyama zaidi  katika eneo hilo na hii inaonesha jinsi gani watu wasivyo na utu mioyoni mwao.

"Inavyoonekana mtu huyu alijifungua halafu akamtupa mtoto huyu, hii ni ajabu sana kwa mtu kubeba mimba miezi tisa halafu kuamua kutupa kiumbe kisicho na hatia" alisema kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja Rajabu

Kwa mujibu wa kijana aliyeona mwili huo alisema alikuwa anaelekea shambani na ndipo alipoamua kupitia sehemu ambayo huwa anaficha jembe na kuona kiumbe huyo akiwa ametelekezwa huku akiwa amekwisha kufa.

"Inawezekana mtu huyu alimtupa mtoto huyu usiku kwani jana wakati naficha jembe hapakuwa na kitu chochote "alisema kijana huyo.

No comments:

Post a Comment