Pages

Pages

Thursday, January 10, 2013

MATEKA 50 WA IRANI WAACHIWA HURU NA WAASI WA SYRIA


Waasi nchini Syria wamewaachia huru raia 50 wa Iran waliowakamata mwaka uliopita, kwa masharti la kubadilisha na zaidi ya raia 2000 wanaoshikiliwa na serikali ya Rais Bashar al Assad.

Raia 48 wa Iran wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la Islamic Revolutionary Guard Corps waliotumwa kupigana upande wa serikali wameonekana katika hotel mjini Damascus wakiwa katika hali nzuri kiafya.

 Iran, mshirika wa karibu wa serikali ya Assad, alisema kuwa watu hao ni mahujaji wa madhehebu ya Shia waliokuja nchini Syria kufanya ibada katika maeneo tukufu.
Wakati huohuo, Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwenye mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi yuko mbioni  kukutana na maafisa wa ngazi za juu wa Marekani na Urusi mjini Geneva kesho Ijumaa.
Mkutano huu unafanyika ikiwa ni siku kadhaa baada ya Rais Assad kutoa hotuba yake ambayo ilitaka kuwepo kwa majadiliano ya amani yatakayomaliza machafuko nchini humo. Hata hivyo Jumatano iliyopita bwana Brahimi aliita hotuba hiyo ya Assad kuwa ni ya kidini na yenye kupendelea upande mmoja.

No comments:

Post a Comment