Pages

Pages

Thursday, January 3, 2013

TUNDAMAN ALIZWA 7ML NA KAHABA WAKIWA FARAGHA


MSANII Tundaman baada ya kumcheka mwenzake Matonya na kumuimba kwenye wimbo wake kuwa alifungiwa ndani na mwanamke na kulizwa shilingi milioni 6, hali kwake imekuwa mbaya zaidi ambapo inadaiwa kuwa hivi karibuni amekombwa milioni 7 na mwanamke mmoja aliyelala naye na kujikuta akiwa hana hata chenji mfukoni.

Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na mwandishi kwa sharti la jina lake kutotajwa kilidai kuwa, msanii huyo alikuwa na sh milioni 7 ambazo alizipata kwenye moja ya show alizofanya hivi karibuni.

Mhabishaji huyo alisema kuwa baada ya kupata kiasi hicho cha pesa alisita kwenda kulala kwa rafiki yake Madee ndipo alipoamua kwenda kwa mwanamke huyo kwa lengo kutunza fedha hizo bila kuchukua tahadhari yoyote na fedha hizo, kitu ambacho kimempelekea kupoteza fedha zote huku mwenyewe akiwa kimya kwa hofu ya kuchekwa.

“Jamaa hadi leo kimya hafanyi tena mchezo wa kwenda kulala na demu na mshiko mrefu kwani kilichomkuta anajuta ni kwa nini alimuimba Matonya kwenye wimbo wake,” kilidai chanzo hicho.

No comments:

Post a Comment