Pages

Pages

Monday, January 14, 2013

WEMA SEPETU NA JB FULL KUKUMBATIANA KILIMO KWANZA DODOMA


Wema Isaac Sepetu na Jacob Steven ‘JB’ wakiwa wamekumbatiana.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri katika Kijiji Cha Kwadelo wilayani Kondoa, Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mastaa hao walikwenda kuzindua mpango wa Kilimo Kwanza, Ajira kwa Vijana ulioongozwa na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati.
Waigizaji hao walionekana kupeana ‘kampani’ kwa kila walichokifanya, huku kila mmoja akigandisha mkono kiunoni kwa mwenzake na kushikanashikana hadharani huku Wema akideka na ‘kale kasauti kake kanakoweza kumtoa nyoka haraka pangoni’.
...Wakiwa pamoja kimahaba.
“Hawa wasanii wetu bwana, hebu waone wale (Wema na JB), muda wote wameshikana vile. Mh! Ndiyo nini sasa?” alisikika mmoja wa maustadhi aliyejitokeza katika uzinduzi huo.
Wakiwa mashambani, ulifika wakati wa mastaa hao kulima kwa kutumia trekta ambapo JB alionekana akimbeba Wema na kumsaidia kupanda kwenye trekta kisha akamsaidia tena kushuka baada ya kumaliza kazi.

No comments:

Post a Comment