Pages

Pages

Wednesday, March 20, 2013

MSANII BONGO MOVIE AHUSISHWA NA KESI YA UJAMBAZI JIJINI DAR

                                                                 
 STAA wa filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga hivi karibuni aliswekwa lupango katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar baada ya kuzushiwa kesi ya ujambazi na mpangaji mwenzake .

Akizungumza na waandishi wetu, Lungi aliyesota mahabusu kwa siku mbili alisema hivi karibuni usiku wa manane aligongewa mlango nyumbani kwake na watu asiowafahamu, alipotoka alikutana na askari waliomchukua na kumwambia kwamba anatuhumiwa kwa ujambazi.

Hata hivyo, Lungi alisema kuwa baada ya kuwauliza askari ni wapi dada huyo amevunjiwa  au kitu gani alichoibiwa, askari walimbadilishia kesi na kumwambia kuwa amemtukana. Mpaka sasa, Lungi yuko nje kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment