WEMA SEPETU AMNUSURU KAJALA KWENDA JELA MIAKA 5
HUKUMU ya kesi iliyokuwa
inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa
leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
jijini Dar.
Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka
mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela
miaka saba au kulipa faini ya shilingi milioni 200.
Kajala
alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe,
Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Mrembo wema sepetu ndo ameweka dau hilo mezani kumnusuru kajala asiendelee kusota kwa kesi ambayo ilikuwa imefikia tamati ya hukumu hiyo.
No comments:
Post a Comment