MTOTO WA MIAKA MINNE ACHOMWA MOTO SEHEMU ZA SIRI KISA UJI
ELIZABETH Bureko (26), mkazi wa Kata ya Nyamatare, Manispaa ya Musoma,
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Musoma, kwa tuhuma
za kumchoma na moto sehemu za siri mtoto wa kike mwenye umri wa miaka
minane. Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Baraka Maganga,
ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Sajini Stephano Mgaya, kuwa
mwanamke huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 24 mwaka huu, saa 3
asubuhi.
Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka huyo, mshitakiwa alikiuka
kifungu cha sheria namba 169 cha mwenendo wa makosa ya jinai kama
sheria hiyo ilivyofanyiwa marekebisho na kuwa namba 16, mwaka 2002.
Alidai
kwamba, mshitakiwa huyo alimchoma katika sehemu zake za siri na
mdomoni baada ya kumtuhumu mtoto huyo wa wifi yake, kwamba alikuwa
akinywa uji wa mtoto aliyekuwa akimnywesha.
Mshitakiwa alikana shitaka na kurudishwa mahabusu hadi Mei 25 mwaka huu, kesi yake itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment