Pages

Pages

Monday, May 13, 2013

NEY NA DIAMOND KUWASHA MOTO DAR LIVE

WASANII wa Muziki wa Kizazi kipya Naseeb Abdul  'Diamond Platinam' na Ney  wa mitego wanatarajia kupanda jukwaa moja kumtafuta nani mkali katika uzinduzi wa video ya Muziki gani itakayozinduliwa Mei 18 mwaka huu katika ukumbi wa Dar LIVE mbagala, Dar ers Salaam.

Uzinduzi wa Video hiyo ambao umeandaliwa na Kampuni ya Yuneda Entertainment inayohusika na masuala ya burudani itawapambanisha wasanii hao ambao kutatafutwa nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva ambapo nyimbo hiyo ya muziki gani inamahadhi ya kubishana kati ya miziki hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, wakati wa kutambulisha uzinduzi huo, Mratibu wa onesho hilo Kahabi Mwendesha alisema uzinduzi huo utasindikizwa na wasanii wa Hip Hop na Bongo Fleva na kuwataka mashabiki wa fike kwa wingi ili kushuhudia wababe hao.

"Onesho hili litakuwa ni la kumtafuta nani mkali kati ya muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva ambapo kupitia uzinduzi wa video hii utadhihirisha nani mkali kati ya muziki wa bongo fleva na hip hop,"alisema Mwendesha.

Alisema mara baada ya video hiyo kuzinduliwa Mei 18 Dar LIVE uzinduzi huo utahahamia katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza, na baadaye Arusha na kuwataka mashabiki wa mikoa hiyo kukaa tayari kwa ajili ya burudani hiyo.

Alisema viingilio katika onesho hilo vitakuwa ni sh. 10,000 huku akisisitiza ulinzi kuimarishwa ambapo pia alisema kwa mashabiki wa burudani ambao hawatakuwa na viingilio kwa ajili ya mechi ya Simba na Yanga wafike katika ukumbi huo kwa kuwa mechi ya watani hao wa jadi itaoneshwa LIVE kupitia televisheni kubwa zilizipo ukumbini hap
o.

No comments:

Post a Comment