Pages

Pages

Tuesday, May 21, 2013

REDD'S MISS TANGA KUJULIKANA JUNI 22 MWAKA HUU






































SHINDANO la mkutafuta malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu "Redd's Miss Tanga 2013" litafanyika Juni 22 kwenye Uwanja wa Mkwakwani,Mkoani humo.

Akizungumza na gazeti hili jana Mkurugezi wa Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula, alisema kuwa warembo tayari wameanza mazoezi yakatofanyika kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.

Kigundula alisema shindano hilo litaanza saa 2, usiku, ikiwa ni pamoja na kuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa moja ya bendi maarufu hapa nchini pamoja na wasanii wanaotamba katika muziki wa kizazi kipya.

Alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri jumla ya warembo 14 watashindania taji hilo.

Kigundula alisema kuwa mpaka juzi warembo 10 wamejitokeza na kuanza mazoezi yanayosimamiwa na  Miss Tanga 2012 Teresia Kimolo na Mwanaid Omar.

Warembo hao ni Hawa Ramadhan (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Jack Emannuel (18),Waida Mmbwambo(20), Tatu Hussein(19), Mwanahamis Mashaka(20), Neema Abdallah (18), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21).

"Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake"alisema Kigundula

Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla wakae mkao wa kupata raha.

Redd's Miss Tanga 2013 imedhaminiwa na Redd's Original,CXC Africa, Executive Solutions,Busta General Supply, Mkwabi enterprises,Lusindic Investment LTD, Lavida Pub, Jambo Leo,Staa Spoti,Five Brothers,Cloud's Media Group,Michuzi Media Group na Blogs za Bongostaz.com, Saluti5, Kajuna, JaneJohn, na Father Kidevu Blog.

No comments:

Post a Comment