Pages

Pages

Monday, June 24, 2013

MISS TANGA 2013 ILIVYOJILI


Miss Tanga 2013, Lulu Ambonea akiwa na washindi wake wa pili, Like Kipenga na mshindi wa tatu Hawa Ramadhani.

Mrembo Lulu Ambonea aliyezaliwa miaka 20 iliyopita, usiku huu ametwaa taji la Miss Tanga 2013 katika shindano lililofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kujinyakulia kitita cha Sh. 500,000 na tiketi ya kushirki shindano la Kanda ya Kaskazini kuelekea Miss Tanzania mwaka huu.
Katika shindano hilo, binti wa kipa wa zamani wa Pilsner ya Dar es Salaam, Abdulrahman Kipenga, aitwaye Like, alikamata nafasi ya pili na kujinyakulia Sh. 300,000 na tiketi ya Kanda, wakati mshindi wa tatu alikuwa Hawa Ramadhani, aliyepata 200,000 na tiketi ya Kanda.
Winfrida Gutram hakuingia tano bora
Irene Thomas.

Miss Talent Hazina Daniel akionyesha ukali wake .
Mrembo Asia Rashid akishindana wakati wa Talent. Shabiki huyu alipanda kumtuza
Warembo wengine wawili walioingia tano bora ni Hawa Twalib na Judith Molel ambao kila mmoja alipata Sh. 100,000 na safari yao inaishia Mkwakwani.
Washiriki wengine saba, kila mmoja alipata Sh. 100,000 wakati mshindi wa taji la Miss Talent, Hazina Daniel alipata 100,000 zaidi kwa kushinda taji hilo.
Hata hivyo, majaji wa shindano hilo walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na watazamaji kutokana na imani kwamba wameboronga.

No comments:

Post a Comment