Pages
▼
Pages
▼
Friday, June 28, 2013
WEMA SEPETU ASHITAKIWA KWA KUCHAFUA MAZINGIRA KIJJITINYAMA
MKURUGENZI wa Kampuni ya Filamu ya Endless Fame, Wema Sepetu hivi karibuni amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya majirani zake kumshitaki kwenye serikali ya mtaa kufuatia tabia ya wafanyakazi wake kutiririsha maji machafu mtaani. Taarifa iliyomfikia mwandishi wa habari hii inadai kuwa, majirani wa Wema katika eneo analoishi, Kijitonyama jijini Dar wamekuwa wakimlalamikia msanii huyo kwa kitendo hicho lakini imeonekana uvumilivu umewashinda.
“Mara kwa mara wafanyakazi wake wamekuwa wakitiririsha maji hapa mtaani sasa leo tumeona tukamshitaki serikali za mitaa ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema mmoja wa majirani wa staa huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Juni 26, mwaka huu Ijumaa lilifika kwenye nyumbani kwa Wema na kushuhudia maji yakitoka kisha kuzagaa mtaani na muda mfupi baadaye alifika Afisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho (jina halikufahamika mara moja) ambaye aligonga kwenye nyumba ya Wema, baada ya muda alitoka binti wa kazi aitwaye Bite.
Katika mazungumzo yao, Bite alionekana kujitetea lakini baadaye ilibainika wana makosa na akatakiwa kwenda ofisi za kata kwa maelezo zaidi.
Amri hiyo ilionekana kuwa ngumu kwa Bite na wafanyakazi wenzake ambapo busara zilitumika na kiongozi huyo wa serikali akataka walipe faini na kuwaonya waache tabia hiyo.
Kufuatia hatua hiyo, Bite aliingia ndani (inadaiwa alikwenda kumtonya Wema) ndipo alipotoka akiwa na fedha ambazo Ijumaa halikujua ni kiasi gani, wakasainishana (angalia picha ukurasa wa pili)kisha mchezo ukaishia hapo.
Jitihada za kumpata Wema kuzungumzia sakata hilo ziligonga mwamba kutokana na msanii huyo kutopokea simu na hata mwandishi alipofika nyumbani kwake aliambiwa hayupo.
No comments:
Post a Comment