Pages

Pages

Monday, July 1, 2013

DIANA LAIZER AWA MISS KANDA YA MASHARIKI 2013

Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2013, Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Ulinzi wa Jamii kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM) ambaye pia ni Malikia wa Taji la Mkoa wa Morogoro Diana Laizer (21) ( kati kati) akiwa na wenzake mshindi wa pili , Sabra Islam (19) ( Kushoto) pia kutoka Mkoa wa Morogoro pamoja na mshindi wa tatu Janeth Awet ( 19) kutokaMkoa wa Lindi mara baada ya kutagazwa washindi katika shindano lao lililofanyika Juni 29, mwaka huu.
Madensa wa Kundi la Msanii wa kizazi kipya Tundaman, wakishambulia jukwaa.

Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, wakiwa katika vazi la jioni.
Mshindi wa nne , Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, Elizabeth Perty kutoka mkoa wa Pwani akipita jukwaani na vazi la ubunifu.

MC katika shindano la kumpata malkia wa Taji la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Kaka Aidan Ricco ambaye ni Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania akielezea utaratibu wa kuwapata washindi watano.

Mshiriki Zulfa Semboja kutoka mkoa wa Mtwara akionesha vazi la ubunifu mbele ya watazamaji

Washindi wanne wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 wakisubiri Jaji Mkuu kutaja majina yao katika nafasi ya ushindi kuanzia kwanza, pili , tatu na ya nne.

Mwanamuziki wa Kike wa kizazi kipya, Keisha ( wa kwanza kulia) akipiga makofi kufurahiamchuano wa warembo wa Redd's Miss Kanda Mashariki , Juni 29, mwaka huu

Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013 yenye taji kishwani akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wenzake waliokuwa wameingia tano bora.

Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2013, Diana Laizer akifurahia kitita cha fedha alichokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa

No comments:

Post a Comment