NANDO ATIMULIWA BIG ROTHER KWA AIBU
Jana
usiku mara tu baada ya Sulu na Annabel kutolewa kwa kura za watazamaji,
Big Brother aliwaita washiriki pamoja katika kikao cha dharura kufuatia
ugomvi uliotokea kati ya Nando na Elikem.
Itakumbukwa kwamba
siku ya ijumaa ilitokea hali ya kutoelewana kati ya Nando na Elikem.
Wawili hawa walitukanana sana na kutishiana mno. Ugomvi huo ulianzishwa
na Nando.
Kwa mujibu wa sheria za Big Brother mwaka huu, kuanzisha ugomvi ni kosa ambalo hupelekea kupata 'strike' ama onyo.
3 strike rule ni mtindo unaotumika msimu huu. Kwa mujibu wa Big
brother, yeyote atakaye fanya makosa matatu makubwa na kupewa maonyo
matatu basi moja kwa moja anatakiwa atimuliwe..
Sheria hiyo
imetumika kumtimua Nando kwa sababu 1. Alianzisha ugomvi siku ya Ijumaa,
2. Alishiriki ugomvi na Elikem na 3. Alitishia maisha, "I feel like
stabbing him. A nigga like that deserves to die"...
Katika
kipindi cha wiki 9 za ushiriki wake katika jumba hilo, Nando amekutwa na
misuko suko kadhaa ikiwemo kuwahi kukutwa na kisu katika Party ya
Channel O pia kukutwa na mkasi chini ya kitanda kitu ambacho ni kinyume
cha sheria za big brother.
Kutokana na ugomvi huo Elikem alipata strike moja.
Big brother alimtaka Nando aondoke katika jumba lake hilo na kutumia
fursa hiyo kuwataka washiriki wengine waishi kama watu wazima.
No comments:
Post a Comment