Pages

Pages

Monday, July 22, 2013

SHILOLE NA SINTA PACHIMBIKA

Akiongea kwa njia ya simu toka nyumbani kwake Sintah baada ya mtandao huu kutaka kueleza anachukuliaje vitosho hivyo vya Shilole ambapo alisema" Kaka naambiwa sana na watu hasa wanaofatilia mitandao eti natafutwa kupigwa na Shilole sasa ninacho shangaa huyo Shilole anapafahamu kwangu aje basi anipige au kwenye ofisi zangu anapajua namkaribisha vizuri sana jamani" Alisema Sintah

Aidha Sintah aliongeza kusema kuwa" Mimi huwa sio mtu wa maneno yeye aje tu anipige na sio kutangaza kwenye mitandao kuwa ananitafuta anipige hayo mambo ya bifu siku hizi watu wanayachukulia upuuzi kutafuta pesa ndio mpango mzima hivyo mimi namshauri Shilole kama underground wa sanaa nchini aachane na bifu badala yake akazane kwenye mambo yake ya kutafuta pesa kwa ajili ya maisha yake na familia kwani uzee unakuja" Alisema Sintah
Chanzo cha ugomvi huo ulitokana na Sintah kuandika habari kwenye mtandao wake kuwa Shilole hawezi kuimba na Jennifer Lopez wa Marekani bora hata Linah wa THT anaweza kufanya hivyo kwa hiyo Shilole aache kuidanganya jamii. Mtandao wa Sintah uliandika hivyo
Aidha Mashabiki mbalimbali hasa wasomaji wa kwenye mitandao wamemuunga mkono Sintah kuhusu kauri yake" Ni kweli jamani Shilole hawezi kuimba na Jennifer Lopez hayo ni masihara jamani kwenda marekani ndio aje kuongea ulojo kiasi hicho kwanza ikumbukwe kuwa wasanii wote wa tanzania kule Marekani hawajulikani hata, hasa kwa sisi tunaofatilia tunajia" Alisema mfanyabiasha wa kimataifa aliyejitambulishia kwa jina la Hamu Juma.

No comments:

Post a Comment