Pages

Pages

Monday, August 19, 2013

BABA AFUMWA NA MWANAE AKILA URODA GESTI



Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Temba, mkazi wa Kimara-Rombo, Dar ambaye ni dereva wa daladala amefumaniwa laivu na mkewe akiwa gesti na binti yao wanayemlea.

Tukio hilo la aina yake lilijiri wiki iliyopita kwenye gesti hiyo iliyopo maeneo hayohayo ya Kimara-Rombo, majira ya saa 10:00 jioni ambapo Temba ambaye ni dereva wa daladala inayofanya safari kati ya Kimara na Kariakoo alinaswa kiulaini baada ya kuwekewa mtego.

Baada ya mke wa Temba kuweka mambo vizuri aliitaarifu wanahabari  ambapo alihojiwa maswali muhimu kisha kutakiwa kuwajulisha polisi ili kuhakikisha kuna usalama wa kutosha.


Kwa mujibu wa mke wa Temba, siku kadhaa nyuma aligundua kuwepo kwa mawasiliano ya kimapenzi kati ya mumewe na binti yao hivyo akalazimika kufanya uchunguzi wa kina.


Mama Temba alisema kuwa katika harakati zake, siku ya tukio alifuma ujumbe wa simu ‘SMS’ kwenye simu ya binti huyo, aliposoma alishtuka kuona ujumbe wa kimapenzi kutoka kwa mumewe.


Kwa kuwa hakuamini alichokisoma, mama Temba ilibidi amwite binti yake ili amweleze vizuri juu ya ujumbe huo.

Alisema kuwa binti huyo (jina linahifadhiwa) mwenye umri chini ya miaka 18, hakuwa na hiyana alimweleza ukweli juu ya tabia ya baba yake huyo kumtaka kimapenzi.

Aliendelea kusema kuwa alipombana kujua kama ‘walishaduu’, binti huyo alidai kuwa amekuwa akimtolea nje.

Mama huyo alisema kuwa hakuwa na papara mara baada ya kuambiwa taarifa hizo, alichokifanya alimtaka binti yake huyo amkubalie na  amwambie baba yake huyo wapange wakutane wapi.


Mama huyo alijifanya binti yake na kuanza kuchati na mumewe masuala ya mapenzi bila kufahamu kuwa anachati na mkewe.
 

Katika kuchati, Temba alituma SMS: “Tulia natafuta mtu wa kumwachia gari (daladala) halafu nitakutumia SMS kukuambia tukutane wapi, leo nataka nifungue ukurasa wa mapenzi na wewe, mwanangu nakuhakikishia utakuwa na maisha mazuri sana.”

Baada ya kukubaliana kukutana gesti hiyo, mama huyo alikwenda kutoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya Kimara-Rombo na kupanga jinsi ya kumnasa.

Majira ya saa 10: 00 jioni, Temba alipata mtu wa kumwachia daladala na kutinga katika gesti hiyo kisha kumtumia SMS binti huyo akimtaarifu ameshafika.

Tofauti na alivyotarajia, ujumbe huo ulitua kwa mkewe ambaye alimwambia binti huyo amfuate mara moja lakini ahakikishe ‘tunda’ halitafunwi.

Ilidaiwa kuwa binti alipofika chumbani alimkuta mtu mzima akiwa amevaa taulo tayari kwa kuvunja amri ya sita na binti yake huyo bila kujua kuwa nje ya nyumba hiyo ya wageni kulikuwa na mkewe na polisi.

Ilisemekana waliachiwa kama dakika kumi na tano ndipo timu nzima ya polisi wakiongozwa na mkewe wakaingia ndani kwani hawakufunga mlango na ‘shughuli’ ilikuwa bado haijaanza.

Habari zilisema kuwa mwanaume alipomuona mkewe anaingia chumbani akiwa ameongozana na polisi nusura apasuke kwa mshtuko kwani alishindwa kuyaamini macho yake.


Ilielezwa kuwa mume alijaribu kutumia kila aina ya lugha kumuomba msamaha mkewe lakini mke aliamuru askari kumtaiti kwa kumpiga pingu na safari ya kwenda kituoni ikaanza.


Kabla ya kupelekwa kituoni jamaa huyo aliibua timbwili zito na kusababisha watu kukusanyika na kuongoza msafara kuelekea polisi huku akitembezwa na taulo mtaani huku mkewe akimbebea nguo nyingine ikiwemo ‘boksa’.
 

“Yaani hata siamini, mume wangu nilimuamini sana kumbe ananizunguka,” alisema mke wa Temba kwa huzuni.
 
Alipofika kituoni, Temba aliandikisha maelezo ambapo hadi mashushushu wetu wanaondoka eneo hilo, kulikuwa na watu kibao waliokuwa wakipiga kelele.

No comments:

Post a Comment