Pages

Pages

Tuesday, August 13, 2013

CHIDI BENZ AKILI KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

 
Rapper Chidi Benz leo kwa mdomo wake mwenyewe amekiri kuwa alikuwa akitumia madawa ya kulevya kwa miaka mingi. Chidi amefunguka leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

Alisema japo hakwenda Nairobi kwaajili ya rehab, mazingira yalimlazimu kutafuta tiba ili aondokane na madhara ya madawa hayo. Alieleza kuwa alipofika jijini Nairobi alikuwa akitakiwa kufanya show nyingi na mwandaaji alimuuliza kama kuna kitu atahitaji ili awezE kufanya show vizuri.

“Nikamwambia Yeah kuna vitu ntavihitaji,” alisema Chidi. “Nikamwambia ‘mimi bana kuna vitu ninavyovitumia nikikaa 20 minutes bila hivyo vitu ni noma nachanganyikiwa na akili tena sina, kwahiyo sijui tutafanyaje’. 

 Akaniambia ‘mimi ntapataje hivyo vitu Chidi na Nairobi ni gharama sana. Nikamwambia ‘mimi pia nina wazo jingine kuna mtu alinitonya kwamba kuna kitu kinaweza kikafanyika na pesa Fulani, pesa nyingi kama milioni 15, 16 hivi za kibongo. 

Akaniambia kikifanyika hicho maanake vinavyofolewa kabisa hivyo vitu vilivyokuwa vinanifanya niwe hivyo. Akaniambia ‘hiyo naijua lakini ni process, ndio maana dunia nzima haifanyi’. Nikamwambia ‘mimi nafanya kwasababu nilishakutwa na vitu vingi mimi ntafanya.”


  Chidi anasema hela hiyo ilipatakana na wakapanga kwenda kufanya mchakato huo wa kuonana na daktari ili kutibiwa.
 
“Kwahiyo mimi sijaenda rehab na wala sijanywa zile methodone sijui watu wanasema watu wanywe methodone.”
Amesema dawa aliyotumia inanunuliwa na mtu huchomwa kama mgonjwa wa kawaida.
 
“Yenyewe inakusafisha wewe pale ambapo ulikuwa ukivuta inakukaa then baada ya dakika kadhaa pakikauka panakuwa pakavu ni kama ile sehemu inakuwa mbichi wewe ukivuta. Huna hela lakini huvuti panakuwa pakavu, pakikauka ndio unachanganyikiwa unaanza sasa kuona alosto lakini kama ukiendelea kuvuta panakuwa pabichi unaendelea. 

So yenyewe inaenda kama mapovu, ni kama sabuni inaenda inakusafisha pale kote panabaki empty. Kwahiyo ni wewe sasa uamue tena kuvuta tena au uache kabisa. Lakini mimi nilienda kusafishwa pote, inakuweka unakuwa na power, inakupa akili, uso rangi, mwili unaanza kubadilika.”

 
Anasema kabla ya kupata tiba hiyo alitakuwa kusaini karatasi kadhaa kuthibitisha kuwa amekubali kupewa dozi.
“Mama yangu pia alikuwa anajua, nilimwambia kwamba mimi bana inabidi nitibiwe.”

  “Niko fresh, niko healthy, nakula vizuri, naishi vizuri, nafikiria vizuri na nimecalm down,” alisema Chidi kuelezea hali yake ya sasa.

Chidi amekiri kuwa alianza kutumia madawa ya kulevya muda miaka mingi iliyopita lakini ilikuwa ngumu wengi kujua kwasababu alikuwa akiutunza vizuri mwili wake.
 
“Naoga vizuri, nakula vizuri, nafanya mazoezi daily, gym daily, kwahiyo hata nikivuta hayanitibui kitu lakini yalikuwa yananijaza tu anger ndani, chuki na ule unoma unoma.”

No comments:

Post a Comment