Pages

Pages

Thursday, August 8, 2013

HOTELI INAYOUZA NYAMA ZA WATU YAGUNDULIKA

Polisi walifanikiwa kuvikamata vichwa hivyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wanaoishi karibu na hoteli hiyo ambapo mbali na vichwa hivyo viwili lakini pia walikamata bunduki mbili aina ya  AK47,kofia mbili za jeshi pamoja na simu nyingi.
Watu saba wanashikiliwa na jeshi la polisi nchini Nigeria katika hoteli moja iliyopo karibu na soko moja maarufu sana nchini humo linalofahamika kwa jina la Ose-Okwodu katika mji wa Anambra baada ya kukamatwa kwa vichwa viwili vya binadamu vikiwa bado vibichi lakini jina la hoteli hiyo linahifadhiwakutokana na sababu za kiusalama

hotel human heads in onitsha 

“kila wakati nimekuwa nakuja hapa sokoni na kufanya biashara zangu katika hoteli hii kwasababu ipo karibu sana na soko.lakini nilikuja kugundua mambo ambayo sio ya kawaida ikiwemo watu wakiingia na kutoka katika hoteli hii,chakushangaza zaidi ni kutokana na watu hao kuwa ni wachafu sana wakati mwingine wakiwa wamechafuka damu,kwahiyo sikushangaa sana kusikia polisi wamegundua unyama huo jana asubuhi”alisema jamaa mmoja muuza mboga mboga katika eneo hilo.

Mchungaji mmoja ambaye ni mmoja kati ya watu waliowatonya askari kuhusu biashara hiyo ya nyama za watu katika hoteli hiyo alisema "niliwahi kwenda kwenye hoteli hiyo mapema mwaka huu,niliagiza chakula lakini baada ya kula nilihisi nyama ilikuwa na chumvi kwa kiwango cha N700,nilishangaa sana.kwahiyo sikujua kama ni nyama ya binadamu au la nilishangaa kwasababu ilikuwa inauzwa ghali sana”alimalizia mchungaji huyo

No comments:

Post a Comment